Wanaume watano wauwawa Moyale, Kenya
Ripoti kutoka Kenya zinasema kuwa askari wa usalama wamewauwa watu
watano wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa kundi la wapiganaji Waislamu wa
Somalia, Al-Shabab, ambao wakijitayarisha kufanya mashambulio ya
kujitolea mhanga.
Msemaji wa ulinzi, (Bogita Ongeri) ananukuliwa akisema kuwa kilo 100 za mabomu na fulana 6 za kuficha mabomu ya kuripua wakati wa kujitolea mhanga, zilikutikana katika gari lao
.
Msemaji wa ulinzi alieleza kuwa watu hao waliwafyatulia risasi askari wa usalama ambao walijibiza kwa kuwapiga risasi na kuwauwa.
0 comments:
Post a Comment