Mwili wa Salome Richard (17) aliyefariki dunia katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema mkoani
Mwanza akidaiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa ebola ulizikwa juzi katika makaburi ya misheni mjini hapa chini ya uangalizi maalumu.
Wataalamu wa afya wilayani Sengerema mkoani Mwanza wakisimamia mazishi ya mgonjwa aliyedaiwa kufariki dunia kwa ugonjwa wenye dalili zinazofananishwa na ebola, |
Hata hivyo, uongozi wa hospitali hiyo umesema hakuna mgonjwa aliyefariki dunia kwa ugonjwa wa ebola na kwamba mgonjwa huyo aliyetoka katika eneo la Nyehunge, alikuwa akisumbuliwa na homa kali.
Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Mary Jose amesema Salome alifikishwa hospitalini hapo Ijumaa saa 4:30 asubuhi akiwa na homa kali.
Amesema muda mfupi baadaye alianza kutokwa na damu puani, mdomoni na sehemu ya haja kubwa, ndipo aliwekwa katika chumba maalumu kwa uangalizi wa madaktari watatu.
CREDIT:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment