WASANII kibao jana
walijitokeza kumuunga mkono msanii Mabeste katika shoo maalum kwa ajili
ya kuchangia fedha za matibabu ya mkewe, Lisa Karl ambaye pia ni meneja
wake.
Shoo hiyo iliyopewa jina la ‘Mrs Mabeste
Charity Show Club 71’ ilifanyika usiku wa jana katika club hiyo iliyopo
Tegeta, jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wasanii waliohudhuria ni pamoja
na Bob Junior, Top In Dar ‘TID’, Ben D, Shebby Love, Sting Wera Wera
toka Kenya na wengineo.
0 comments:
Post a Comment