Wakazi wa Ilula Mkoani Iringa wamegoma kupokea maiti ya mama aliyeuwawa wakati wa mapambano yalioyotokea juzi mkoani Iringa kati yao na polisi kwa masharti mawili:
Mosi: Wananchi 18 Waliokamatwa na jeshi la polisi baada ya vurugu hizo waachiwe mara moja bila masharti yoyote.
Pili: Polisi walio sababisha mauaji hayo wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria .
Katika tukio hilo, wananchi wa Ilula walimtuhumu polisi kumuua mwanamke kwa kosa la kuuza pombe muda wa kazi na hivyo kupanda ghadhabu na kuvamia kituo cha polisi ambako walichoma magari matano madogo na basi moja na baadaye kwenda kufunga Barabara ya Dar es Salaam- Mbeya kwa muda wa saa tano hadi Jeshi la Polisi lilipoongeza askari wake kutuliza ghasia hizo

0 comments:
Post a Comment