MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Rashidi Makwilo maarufu
kama ‘Chid Benz’, aliyekuwa anatuhumiwa kwa kukutwa na dawa za kulevya
aina ya heroin na bangi, leo ameachiliwa huru kwa kulipa faini ya Sh.
900,000.
Katika maelezo ya awali yaliyosomwa na mwendesha mashtaki wa Jamhuri
Diana Lukendo, mbele ya Hakimu Warialwande Lema, msanii huyo alimwambia
hakimu kuwa mshtakiwa alikamatwa na dawa hizo za kulevya akiwa Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, akitaka kusafiri
kuelekea mkoani Mbeya.
Hata hivyo mshtakiwa huyo ambaye alikiri kosa mnano tarehe 18 Aprili mwaka huu, leo aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu na kwamba asingetumia tena ulevi huo na atawaelimisha vijana wenzake juu ya madhara yake.
CHID mwenyeshati jeupe wakati akitoka mahakama ya kisutu akiwa mtu huru |
Hata hivyo mshtakiwa huyo ambaye alikiri kosa mnano tarehe 18 Aprili mwaka huu, leo aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu na kwamba asingetumia tena ulevi huo na atawaelimisha vijana wenzake juu ya madhara yake.
0 comments:
Post a Comment