Mashabiki wa mwanamasumbwi nguli wa
kitambo Mike Tyson wana tatizo moja kubwa,ni namna gani wanaweza
kujipiga picha pamoja naye? Na hata ukipata bahati ya kupiga picha
pamoja naye uhakikishe hutamuudhi, ni jambo ambalo halitabiriki.
Mmoja
wa watu wanaomfakilia Mike Tyson,aliamua kubwia funda kadhaa za pombe
ili auvae ujasiri na aijaribu bahati yake na kumkaribia mkali huyo wa
ulingo ili apate picha binafsi, lakini bahati haikuwa yake. Tukio
hili halikutokea kitambo ni juzi kati tu wakati wa pambano kubwa
lililoukamata ulimwengu na kuwa na kiu inayofanana ya kushuhudia nani
mbabe kati ya Floyd Mayweather na Manny Pacquiao na hatimaye tajiri
Mayweather ambae jina lake la utani ni Money, alipokea zaidi ya dolla
millioni $150m na Pacquiao kuambulia millioni $100m.,video hiyo ilinaswa
kwenye picha za video na kuzunguuka dunia na inamuonesha Tyson akiwa
katika taharuki na kung’aka kufuatia kuchukuliwa poa . Mwanamasumbwi
huyo nguli wa zamani ulingoni ambaye sasa ana miaka arobaini na nane
ambaye kwa hiari yake aliamua kustaafu kuvurumisha ngumi zenye uzito wa
kilo mia mbili,alionekana akigeuza shingo yake kwa mshangao ,wakati
shabiki wake alipokuwa katika harakati za kujipiga picha huku
akihakikisha mkali huyo yumo kwenye picha hiyo,na kabla shabiki huyo
hajazidi kumkera na kuonekana sugu kuelewa vitendo vya Tyson kuwa
anakereka kwa vitendo vyake. Pamoja na mkali huyo kumuashiria
kumpotezea naye kutotaka kuonekana kwenye picha hiyo,Tyson sasa akaanza
kurusha kiwiko chake cha mkono ili kumlazimisha shabiki wake huyo
kuachana na jaribio hilo
0 comments:
Post a Comment