Simba na Mtibwa Sugar Leo zitacheza Fainali ya Mapinduzi Cup 2015 kwenye Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar.
Hii itakuwa mara ya pili kwa Timu hizi kukutana kwenye Mashindano haya kwani walikuwa Kundi moja na hapo Januari Mosi Mtibwa Sugar iliifunga Simba 1-0 ikiwa ni mwendelezo wa uteja wa Vigogo hao wa Tanzania toka kwa Timu hiyo ya Manungu, Morogoro.
Hata hivyo, Simba baada ya kupokea kichapo hicho ilijikongoja na kutinga Fainali kwa kushinda Mechi zao za Kundi lao zilizobaki kwa kuzifunga 1-0 Mafunzo na JKU na Robo
Fainali kuinyuka Taifa ya Jang’ombe 4-0 kisha Nusu Fainali kurudia ushindi wa 1-0 dhidi ya Polisi ya Zanzibar.
Mtibwa Sugar wao, baada ya kuifunga Simba, walitoka 1-1 na JKU na 0-0 na Mafunzo na
kwenye Robo Fainali kutoka 1-1 na Azam FC na kuibwaga kwa Penati 7-6 kisha Nusu Fainali walitoka 0-0 na JKU na Mtibwa kusonga kwa Mikwaju ya Penati 4-3.
+++++++++++++++++++
RATIBA/MATOKEO:
**Saa za Bongo
** Mechi zote kuchezwa Uwanja wa Amaan
Alhamisi Januari 1
JKU 2 Mafunzo 0
Polisi 1 Shaba 0
Simba 0 Mtibwa 1
Ijumaa Januari 2
KMKM 0 Mtende 0
KCCA 2 Azam FC 2
Yanga 4 Taifa ya Jang’ombe 0
Jumamosi Januari 3
JKU 1 Mtibwa 1
Mafunzo 0 Simba 1
Jumapili Januari 4
Yanga 4 Polisi 0
KCCA 3 Mtende 0
Taifa ya Jang’ombe 1 Shaba 0
KMKM 0 Azam FC 1
Jumatatu Januari 5
Mtibwa 0 Mafunzo 0
Simba 1 JKU 0
Jumanne Januari 6
KCCA 2 KMKM 1
Polisi 0 Taifa ya Jang’ombe 0
Azam FC 1 Mtende 0
Yanga 1 Shaba 0
Jumatano Januari 7
Robo Fainali
Simba 4 Taifa ya Jang’ombe 0
Alhamisi Januari 8
KCCA 0 Polisi 0 [Penati 4-5]
Azam FC 1 Mtibwa Sugar 1 [Penati 6-7]
Yanga 0 JKU 1
Jumamosi Januari 10
Nusu Fainali
Simba 1 Polisi 0
Mtbwa Sugar 0 JKU 0 [Penati 4-3]
Jumanne Januari 13
Fainali
2015 Simba v Mtbwa Sugar
0 comments:
Post a Comment