
Kuna
mijengo kibao ya thamani ya wanasoka, lakini hapa tunakuletea mijengo
10 iliyo na thamani zaidi, hebu itupie macho a moja baada ya jingine.
1. David Beckham: $20 million

David
Beckham anamiliki mijengo kibao ya gharama, mmoja kati ya hiyo ni ule
alioupa jina la “Beckingham Palace” uliopo katika Jiji la London
ukiripotiwa kuwa na thamani ya dola milioni 20. Aliununua mwaka 1999.
Pamoja na mambo mengine, una chumba cha kufanyia ibada, studio ya
kurekodia muziki na uwanja wa soka.
2. Wayne Rooney: $17.83 million

Wayne
Rooney anayeishi katika eneo la Cheshire katika Jiji la Manchester
akiwa jirani na nyota wenzake kama Robin van Persie na Rio Ferdinand,
mjengo wake una thamani ya karibu dola milioni 17.83 – kiwanja peke yake
kina thamani ya dola milioni 1.57. Mjengo huo uliojengwa mwaka 2004,
una bwawa kubwa la kuogelea, ukumbi binafsi wa burudani, eneo la sanamu
za utamaduni wa kigiriki, na mfumo maalumu wa kutengeneza joto ardhini
wakati wa barini katika bustani. Wazza pia amefunga kamera zenye mfumo
wa kurekodi kwa siri matukio mbalimbali (CCTV) kwa thamani ya karibu
dola 48,800.
3. Didier Drogba: $9 million

Didier
Drogba mwenye utajiri wa dola milioni 20.8 kwa mujibu wa Forbes,
anamiliki mjengo wenye thamani ya dola milioni 9 uliojengwa mwaka 2007
ukiwa kwenye eneo la mita za mraba 799. Una bafu nane, vyumba vya saba
vya kulala na chumba cha kuwekea mataji.
4. John Terry: $7.5 million

Kwa
sasa, John Terry bado ni mchezaji maarufu wa Chelsea licha ya kustaafu
kuichezea timu ya taifa ya Uingereza. Anamiliki mjengo wenye thamani ya
dola milioni 7.5, ambao ulikuwa sokoni huko nyuma. Una ukumbi binafsi wa
sinema wenye uwezo wa kuchukua watu 34 na vyumba 10 vya kulala.
5. Frank Lampard: $7 million

Nyota
wa zamani wa Chelsea anayecheza kwa mkopo Manchester City, Frank
Lampard anamiliki mjengo wenye thamani ya dola milioni 7 ukiwa kwenye
eneo la mita za mraba 1,812. Mjengo huu una vyumba tisa vya kulala, bafu
12, uwanja wa gofu, bwawa la kuogelea, uwanja wa tenisi na hata kizimba
cha boti.
6. Cristiano Ronaldo: $6 million

Mjengo
wa Cristiano Ronaldo ulio katika Jiji la Madrid aliununua mwaka 2008
kwa bei ya dola milioni 6. Una gym, pool, sauna, gym, bwawa la kuogea,
sehemu maalumu ya kuhifadhia samaki kwa ajili ya kujiburudisha kwa
kuwatazama na ukumbi binafsi wa burudani.
7. Mario Balotelli: $4.86 million

Kwa
sasa Mario Balotelli haishi katika mjengo huu wenye thamani ya dola
milioni 4.86. Ameupangisha kwa pango ya dola 21,930 kwa mwezi baada ya
kuondoka Manchester City kwenda AC Milan mwaka jana. Mjengo huu una
bwawa la kuogelea, baa, ukumbi binafsi wa burudani, uwanja wa kuchezea
gofu, vyumba vinne vya kulala na vya kuogea.
8. Andres Iniesta: $4.6 million
Staa
huyu wa Barcelona na Hispania anamiliki mjengo wenye thamani ya dola
milioni 4.6. Mjengo huu unaonekana mdogo kwa nje, lakini kwa ndani ni
tofauti: una vyumba vitano vya kulala, bwawa la kuogelea na chumba cha
kufanyia ibada ikizingatiwa kuwa ni muumini wa Kanisa Katoliki.
9. Kaka: $3 million

Ricardo
Izecson dos Santos Leite – maarufu kwa jina la Kaka – ana mjengo ulio
katika mita za eneo 139.4 jijini Madrid ukiwa na thamani ya dola milioni
3. Aliununua mwaka 2009 baada ya kujiunga na Real Madrid akitokea AC
Milan. Pamoja na mambo mengine, una gym, bwawa la ndani la kuogelea,
gereji yenye uwezo wa kuhudumia magari sita kwa wakati mmoja. Kwa sasa
ameupangisha kwa supastaa wa Real Madrid, Gareth Bale kwa pango ya dola
16,000 kwa mwezi.
10. Lionel Messi: Thamani haijulikani

Mjengo
wa Lionel Messi thamani yake haijawekwa wazi, lakini unastahili
kumilikiwa na watu wa hadhi yake. Una spa, ukumbi binafsi wa burudani,
uwanja wa ndani wa soka. Kwa sasa staa huyo ana mpango wa kujenga mjengo
mpya wa kifahari ambao ramani yake ni kama uwanja wa soka unavyoonekana
kutokea juu (tazama picha hapo chini).

0 comments:
Post a Comment