Mahakama Kuu ya Mkoa wa Mwanza imetengua kifungo kwa mzazi
mwenzake na Nay Wamitego, Siwema kwa kumhukumu kifungo cha nje cha miaka
miwili.
Mwezi April mahakama kuu ya Mkoa wa Mwanza ilimhukumu Siwema kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na kesi kumtukana matusi kwa njia ya mtandao mlalamikaji ambaye anafahamika kwa jina la Deo.
Akiongea na Bongo5, Nay Wamitego amesema, “Ndiyo ana kifungo cha nje, nimemsaidia kama mzazi mwenzangu sijawahi kufikiria kurudiana naye. Nimefight mimi na ndugu zake ilimradi nitimiza kile ambacho niliwaahidi watu kile ambacho nilizungumza.”
Aidha Nay wa Mitego ameongeza kuwa ameonana na mzazi mwenzake huyo siku ya mwisho tangu amefungwa na wala hana mawasiliano naye tena kwa kukwepa kuanzisha mambo mengine yasiyokuwa na msingi.
0 comments:
Post a Comment