Polisi mkoani Tanga inamshikilia Gladness Daniel (18) mkazi wa Kijiji cha Kwekivu kata ya Kibirashi wilayani Kilindi mkoani Tanga kwa tuhuma za kumkata mkono mume wake kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.
Akizungumza katika kikao cha hali ya uhalifu
mkoani Tanga kilichowashirikisha maofisa usalama barabarani jana,
Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Fraisser Kashai, alisema tukio hilo
lilitokea juzi saa 8 usiku wakati mume wa mke huyo akiwa amelala.
Alimtaja majeruhi huyo kuwa ni Sharif Suleiman(25)
ambaye ni mfugaji alikatwa mkono wa kushoto kwa silaha aina ya shoka na
usiku huohuo mtuhumiwa kudaiwa kutoroka kwenda kwa shangazi yake
anayeishi kijiji cha Songe.
Alisema uchunguzi wa awali wa kipolisi umebaini
kuwa wawili hao walikuwa katika misigano ya ndoa kwa muda mrefu na kila
mmoja alikuwa akimtuhumu mwenzake kwa kukosa uaminifu.
Kamanda Kashai alisema majirani walisema kuwa
wenza hao kila siku walikuwa wakipigana na kutuhumiana kwa kila mmoja
kumwendea mwenzake kinyume.
SOURCE;MWANANCHI
SOURCE;MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment