Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Friday, November 7, 2014

MPYA:WHATSAPP YAWEKA ALAMA KUONYESHA UJUMBE UMESOMWA NA NA SA NGAPI UMESOMWA

Whatsapp wamewapunguzia sababu ya kujitetea wale wote wenye tabia za kutojibu message kwa kisingizio kuwa hawakuziona hata kama zilionesha tiki mbili kuashiaria zimefika. Sasa Whats App imeongeza alama ya kuonesha kuwa ujumbe umesomwa na muda ambao umesomwa.
Whatsapp1
Kuanzia sasa ujumbe ambao tayari umepokelewa na kusomwa utakuwa unaonesha tiki mbili za blue upande wa kulia chini kwenye simu ya mtumaji, na uki bonyeza juu ya ujumbe huo itakuwa ikionesha muda ambao ujumbe huo ulisomwa.
whatsapp2
Kabla ya maboresho hayo kulikuwa na aina mbili tu za tiki, tiki moja ya kijivu ilikua ikionesha ujumbe umetumwa, tiki mbili za kijivu ziliashiria ujumbe umefika.
whatsapp-3
Upande wa messages za group, tiki mbili za blue zitakuwa zikionekana pindi tu watu wote kwenye group wakiusoma ujumbe.
Ili kuona mabadiliko hayo, mtumiaji wa Whatsapp anapaswa ku update app hiyo kwenye simu yake.

Related Posts:

0 comments: