Muonekano wa Balozi wa Marekani nchini Korea Kusini, Mark Lippert baada ya kuchomwa kisu
BALOZI wa Marekani
nchini Korea Kusini, Mark Lippert ameshambuliwa kwa kisu usoni na katika
kifundo cha mkono wake leo na mshambuliaji aliyekuwa anapinga mazoezi
ya kijeshi ya Korea Kusini na Marekani.
Mara tu baada ya shambulio hilo Rais wa Marekani Barack Obama
amemtakia uponaji wa haraka msaidizi wake wa zaman, Mark Lippert,
akimuombea uponaji wa haraka baada tu ya shambulio lililofanywa wakati
wa hotuba ya asubuhi.Balozi huyo mwenye umri wa miaka 42 alikimbizwa hospitalini ambako alifanyiwa upasuaji wa zaidi ya saa mbili ingawa madaktari wamethibitisha majeraha yake hayahatarishi maisha yake.
Jeraha lake limekadiriwa kuwa na sentimeta kumi na moja upande wa kushoto na ameshonwa nyuzi themanini kwenye mkono uliokatwa katika shambulio lililosababisha baadhi ya mishipa kushindwa kufanya kazi. Msemaji wa Ikulu ya Marekani amelaani kitendo hicho kwa nguvu zote.
Baada ya shambulio hilo maofisa wa polisi walionekana wakimrukia na kumdhibiti mshambuliaji aliyekuwa na kisu chenye urefu wa inchi kumi.
Polisi wamemtambua mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 55 aitwaye Kim Ki-Jong, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya shambulio kama hilo kwa kumshambulia balozi wa Japan nchini Seoul mnamo mwaka 2010.
Mkuu wa polisi Yoon Myung amesema kwamba wanamshikilia mtuhumiwa huyo na wanachunguza sababu ya shambulio hilo na masuala mengine.
0 comments:
Post a Comment