Kilimo ni
uti wa mgongo kutokana na kwamba watanzania waliowengi ni wakulima lakini
tatizo kubwa ambalo limekuwa likiwakabili wakulima hawa ni uhaba wa mbolea na
pembejeo
Hata hivyo
mbolea ambazo zimekuwa zikitolewa kwa njia ya ruzuku zimekuwa zikitafunwa na
baadhi ya watendaji ambao siyo waminifu, pia wakibainika na ubadhirifu huo
huhamishwa kutoka ofisi moja hadi nyingine.
Afisa wa takukuru mkoani iringa bw. Ismail Bukuku alisema viongozi wenye tabia ya
kutafuna mali za serikali wakamatwe kama wala rushwa na siyo kuhamishwa kutoka
sehemu moja hadi nyingine.
Na mbolea
ambayo imekuwa ikitumiwa na wakulima ni mbolea ya minjingu ambayo hulalamikiwa
na wakulima walio wengi kuwa haina ubora.
Wadau wa
kilimo wameshauriwa kutoa elimu mara kwa mara kuhusu matumizi bora ya mbolea ya
minjingu ili wakulima wafanye kazi kwa utaramu na siyo kubahatisha “Ameria
galinoma diwani wa kata ya kalenga alisema,” kwa upande wake afisa kilimo
wilaya ya Iringa Lucy nyalu alisema, elimu kuhusu matumizi ya mbolea ya minjingu
imekuwa ikitolewa kupitia mashamba darasa.
Hata hivyo
mwenyekiti wa kamati ya pembe jeo ambae pia ni mkuu wa wilaya ya Iringa Dr.
letisia warioba alisema vikundi vitakavyo kopeshwa mbolea ni vile vilivyo
sajiliwa tu, pia amewataka madiani wawahamasishe wananchi kujisajiri katika
vikundi mbalimbali.
Aidha
warioba aliahidi kutoa milioni moja (1) kwa wilaya ya iringa ili isaidie ujenzi
wa maabara.
0 comments:
Post a Comment