Mchezaji wa timu ya taifa ya England ambaye pia anakipiga katika klabu
ya soka Sunderland Adam Johnson amekamatwa na polisi kwa tuhuma za
kufanya mapenzi na msichana mwenye umri wa miaka 15. Polisi katika eneo
la Durham wamesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amekamatwa
mapema wiki hii kwa tuhuma za kufanya ngono na binti mwenye umri wa
chini ya miaka 16, na amebaki chini ya ulinzi. Taarifa ndani ya klabu
yake zinasema kuwa mchezaji huyo amesimamishwa kusubiri matokeo ya
uchunguzi wa polisi. Taarifa za kukamatwa kwake zilitolewa mapema
kupitia gazeti la The Sun. Kukamatwa kwake kunakuja muda mfupi kabla
hajasafiri na timu yake ya Sunderland kwenda kukutana na Hull kwa
michezo ya Ligi kuu ya England iliyopangwa kuchezwa leo usiku.
Sunderland imesema haitaendelea kuzungumzia kukamatwa kwa mchezaji wake.
CHECK me!!!!
Tuesday, March 3, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment