Baadhi ya majirani wa mtaa wa Hayanga RRM jijini Mbeya wakiwa nje ya nyumba ambapo tukio hilo limetokea . |
Waombolezaji |
Watu wawili wafanyakazi shirika la Umeme Tanesco Mkoa wa Mbeya Ndugu
Uswege Mwankuge (58) na Jusio Uswege (48) ambao ni mtu na mke wake wamekutwa
wamekufa ndani ya nyumba yao mtaa hayanga RRM jijini mbeya .
Tukio hilo la kusikitisha
limetokea leo jijini hapa ambapo inadaiwa kuwa wawili hao wamekutwa wamekufa ndani
ya nyumba yao usiku wa kuamkia leo Marchi 3 mwaka huu
Akizungumiza tukio hilo
Balozi wa mtaa huo Jofrey Katuli amesema yeye alipigiwa simu majira ya saa 4
asubuhi kuwa Ndugu Uswege Mwankuge
pamoja na mke wake ndugu Jusio Uswege wamekufa wakiwa ndani ya nyumba yao .
Amesema watoto wa marehemu ndio waliogundua
kuwepo kuwepo kwa tukio hilo kutokana kuwepo kwa
ukimywa wa muda mrefu ndani ya chumba cha wazazi wao ambapo walilazimika kuingia
chumbani na kumkuta baba na mama yao tayari wakiwa wamekufa .
Amesema baada ya kugonga kwa
muda mrefu bila kufunguliwa walilazimika kubomoa mlango ambapo walikuta baba
yao akiwa amening'inia juu huku tayari akiwa amekufa kwa kujinyonga ambapo
mama naye alikuwa amelala kitandani huku
akiwa amekwisha fariki ambapo mwili wake ukiwa na majeraha shemu za usoni.
0 comments:
Post a Comment