Timu ya Taifa ya Tanzania ikiwa katika jezi zake za awali za bluu iliyokolea na alama za njano na nyeusi na kijani |
Shirikisho
la soka Tanzania, TFF, limesema linakaribisha wabunifu watakaobuni
mwonekano wa jezi mpya za timu ya taifa kwa mechi za nyumbani na
ugenini.
Hata hivyo sharti la ubunifu huo lazima uzingatie rangi za bendera ya taifa ambazo ni kijani, njano, nyeusi na bluu.Wakati tangazo hili likitolewa na TFF, tayari uongozi mpya chini ya rais wake Jamal Malinzi umebadili jezi zinazotumiwa katika mechi za timu ya taifa, Taifa Stars, kutoka zile zilizozoeleka na mashabiki na Watanzania wote hadi jezi mpya zinazolalamikiwa na mashabiki wengi kuwa hazina mvuto na hazionyeshi rangi halisi ya bendera ya taifa la Tanzania.
Jezi mpya ya timu ya taifa ya Tanzania, ambayo nayo inatakiwa kubadilishwa |
Mbunifu atakayeshinda atapata zawadi ya shilingi milioni moja za Kitanzania sawa na karibu dola mia saba za Kimarekani kwa atakayebuni jezi ya kuchezea mechi za nyumbani na vile vile mshindi atakayebuni jezi za kuchezea mechi za ugenini naye atapata kiasi kama hicho cha fedha.
Jezi ya sasa ina rangi ya samawati na bluu nyeusi.
0 comments:
Post a Comment