Mfuko wa
pesheni wa PSPF umetoa msaada wa bati mia mbili (200) zenye thamani y ash.
Milioni sita (6) za kitanzania kwa mkuu wa wilaya ya kilolo Bw. Gerrad
Gurninita ambazo zitasaidia ujenzi wa maabara.
Makabidhiano
hayo ya bati yalifanyika hapo jana mbele ya viongozi wa PSPF na waandishi wa
habari katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya kilolo.
Gerard Guninita |
Aidha mkuu
wa wilaya ya Kilolo gerrad gurninita alisema msaada huo utasaidia kukamirisha
ujenzi wa maabara katika shule zote za sekondari ambapo wanatarajia kukamirisha
ujenzi huo ifikapo 30 novemba 2014
Guninita aliongeza
kuwa miongoni mwa shule zitakazonufaika na msaada huo ni shule ya sekondari ya kiheka,
iketa pamoja na shule ya sekondari ya lulanzi.
Pia alisema
shule ambazo zimeshakamirisha ujenzi wa maabara ni shule ya sekondari ya madege
iliyopo kata ya idete, masisiwe, mawambala, na shule ya sekondari ya kilolo
lakini kwa upande wa shule ya lulanzi wameanza kujenga msingi.
Hata hivyo guninita
aliwataka wananchi kuunga mkono katika ujenzi huo wa maabara kwa kutoa chochote
walichonacho.
0 comments:
Post a Comment