Msimu
uliopita ulikuwa mbaya sana kwa Manchester United katika historia yao
ya Premier League, lakini bado haikuwazuia kuwa matajiri zaidi miongoni
vilabu zilizotengeneza pesa nyingi duniani.
Katika orodha mpya ya iliyotoka wiki hii, United ni klabu ya pili kwa utajiri duniani ikiwa nyuma ya Real Madrid.
Klabu
hiyo ya Old Trafford imeziacha nyuma timu mbili zenye nguvu barani
Ulaya, Barcelona na Bayern Munich ikiwa imeongeza mapato yake kutoka
pauni milioni milioni 363.2 hadi 433.2.
Ligi Kuu ya England imetesa sana katika orodha hiyo ambapo katika timu 30 tajiri duniani, ligi hiyo imeiingiza timu 13.
Manchester
City ni ya sita ikifuatiwa na Chelsea, Arsenal na kisha Liverpool huku
Totteham ikishika nafasi ya 13, Newcastle ni ya 19 na Everton imekamata
nafasi ya 20.
Orodha kamili ya timu 30 tajiri duniani kwa msimu wa 2013/2014 ni hii hapa.
1. Real Madrid - £459.5m
2. Manchester United - £433.2m
3. Bayern Munich - £407.7m
4. Barcelona - £405.2m
5. Paris Saint-Germain - £396.5m
6. Manchester City - £346.5m
7. Chelsea - £324.4m
8. Arsenal - £300.5m
9. Liverpool - £255.8m
10. Juventus - £233.6m
11. Borussia Dortmund - £218.7m
12. AC Milan - £208.8m
13. Tottenham - £180.5m
14. Schalke 04 - £178.9m
15. Atletico Madrid - £142.1m
16. Napoli £137.8m
17. Inter Milan - £137.1m
18. Galatasaray - £135.4m
19. Newcastle United - £129.7m
20. Everton £120.5m
21. West Ham United - £105.3m
22. Aston Villa - £101.9m
23. Marseille - £100m
24. Roma - £97.7m
25. Southampton - £97.3
26. Benfica - £96.6
27. Sunderland - £95.7m
28. Hamburg - £92.2m
29. Swansea City - £90.5m
30. Stoke City - £90.1m
0 comments:
Post a Comment