Mchezaji wa mpira wa vikapu LeBron James alivunja protokali au kuvunja kanuni za maadili ya kifalme alipomshika mabegani Kate Middleton akiwa na majasho kwenye jezi lake huku mumewe Kate, Prince William akifanya mzaha kuhusu ukubwa wa mguu wa mchezaji huyo huku wote wakiangua kicheko.
Haya yalitokea punde baada ya mechi ya mpira wa vikapu ambayo Prince William na mkewe mjamzito Kate Middleton walishuhudia mjini New York wakati wakipigwa picha za pamoja.
Prince William na Kate walipigwa picha baada ya mechi kati ya Cleveland Cavaliers mjini New York Jumanne walipkuwa wakicheza na Brooklyn Nets, ambapo walikabidhiwa jezi ya mwanao mwenye umri wa mwaka mmoja Prince George.
Lakini kamera zilipokuwa zinapigwa, James aliweka mkono wake kwenye bega la Kate na kuvunja kanuni za maadili ya kifalme, licha ya kujulikana kwa jina la mzahaha kama King James.
Baada ya tukio hilo, wawili hao walikwenda kukutana na wanamuziki mahiri duniani Jay-Z na mkewe Beyonce kupigwa picha nyingine.
Lakini je unahisi kuwa mchezaji LeBron alivunja kanuni za kifalme kwa kumsika Kate begani?
0 comments:
Post a Comment