Msitu wa Amazon |
Mtaalamu
wa masuala ya hali ya hewa ameiambia BBC kuwa kuna uhusiano mkubwa kati
ya uharibifu wa mazingira katika msitu wa Amazon na mfululizo wa ukame
nchini Brazil.
Sao Paulo |
Takwimu zinaonye kuwa ukame huo umekuwa na madhara makubwa katika mji mkubwa nchini Brazil wa Sao Paulo.
Dr. Antonio Nobre ambaye ni mtaalamu wa hali ya hewa amesema vyanzo vya maji vinaweza kutoweka na kusababisha madhara kwa zaidi ya watu milion 20 iwapo hali hiyo ya uharibifu katika msitu wa Amazon hautadhibitiwa.
Baada ya kuwa ndani ya ukame kwa zaidi ya miaka nane mfululizo kina cha maji kwa sasa mjini Sao Paulo kipo katika hali ya hatari.
Serikali nchini humo iansema imelazimika kuanzisha mgao wa umeme kutokana na uhaba wa maji ikiwa ni moja ya hatua za dharula.
0 comments:
Post a Comment