Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Thursday, October 30, 2014

FRANSIS CHEKA : Kuokota chupa kunanilipa kuliko masumbwi

Bingwa wa zamani wa dunia wa WBF, Francis Cheka ameamua kujikita zaidi kwenye kazi yake ya kuokota chupa ambayo amedai inamwingizia pesa nyingi kuliko ngumi.
cheka+clip
Cheka akiwa kwenye furushi lake ya chupa


Cheka ameliambia gazeti la Mwananchi kuwa alianza biashara hiyo 2004 baada ya kuamua kuingia mtaani kuokota na kuziuza mwenyewe, wakati huo kilo moja iliuza shilingi 100.
“Nilipoanza kucheza mapambano ya ubingwa wa Afrika nilisimama kuokota chupa nikawaachia wengine na mimi kuelekeza nguvu zangu kwenye ngumi, kijiwe changu nikamweka mtu wa kufanya hiyo kazi na nikawa na nanunua kwa watu wengine kisha mimi nauza tena,” alisema.
“Kwa kipindi chote ambacho nilikuwa nimebanwa na masuala ya ngumi, mradi wangu huu uliyumba kwani kila niliyemwachia alikuwa na fikra za kuniibia, ilifikia mahali nikakwama kwani nilikopa fedha benki kuongezea nguvu kwenye biashara yangu ya makopo hivyo nilipaswa kulipa.”

Related Posts:

0 comments: