Vijana,
wadau na wanaharakati wamefungua vikundi vya mtandao wa kijamii kwa
ajili ya kuchanga fedha za kumsaidia kijana wa Arusha aliyepatikana na
hatia ya kumtukana Rais na kuhukumiwa faini ya Sh7 milioni au kifungo.
Kijana
huyo, Isaack Habakuki wa Arusha alipatikana na hatia ya kumtukana Rais
kwa kutumia ukurasa wake wa facebook na ametakiwa kulipa fedha hizo kwa
awamu mbili na kuzikamilisha ifikapo Julai 7 au kwenda jela miaka
mitatu.
Diwani
wa Kata ya Levolosi jijini Arusha (Chadema), Ephata Nanyaro ambaye
anaratibu michango hiyo kwa mkoa wa Arusha, alisema mpaka sasa
wameshakusanya Sh 800,000/- ambazo walizipata kwa njia ya kutuma kwa
simu.
Alisema wanatarajia kupata Sh1.7 milioni kutoka mikoa yote.
"Tumesikia
familia yake imeweza kutoa 3.5 millioni pekee, sisi tumejitolea
kumsaidia ili afikishe 7 millioni kabla ya tarehe 7 mwezi julai,” alisema.
0 comments:
Post a Comment