Rapper Nay wa Mitego amesema wasanii wachanga wanajisikia ufahari kutoka kimapenzi na mastaa wa kike wenye umri mkubwa.
Akizungumza katika kipindi cha Enewz cha East Africa Television Alhamisi hii, Nay wa Mitego amesema kuwa wasanii wachanga hawawezi kujizuia kutoka kimapenzi na mastaa wa kike waliyowazidi umri kwa kuwa walikuwa wanawatamani kwa muda mrefu.
“Mimi siwezi kuwalaumu hao vijana kuwa na uhusiano nao, unaju inaweza kuwa mtaani siku moja ulikuwa unawishi siku moja kuwa na mtu fulani, halafu ikitokea nafasi kama ile pale aah! Mtu hata upewe ushauri wa dizaini gani mtu ambaye ulikuwa ukimuona kwenye runinga anaingia katika kumi na nane zako mimi siwalaumu japokuwa wanatakiwa kuwa makini”, alisema Nay
Pia Nay alisema wasanii wengi wa kike, wamekuwa wakiutumia udhaifu huo ili kutembea na wasanii wachanga.
0 comments:
Post a Comment