Lakini kadri uhusiano huo unavyozidi kukomaa na kuanza kuitana wapenzi
au wenza ndipo ukweli unapojidhihirisha kuwa hamko wenyewe katika dunia
hii bali pia kuna watu wengine.
Sasa hapo ndipo huwa na tatizo, je, hao watu wengine wanaolizunguka
penzi lenu ni wa kuogopwa? Wanahatarisha kitu chochote katika uhusiano
wenu?
Tunapokuwa katika uhusiano uliokomaa, mara nyingi tunadhani kuwa
muunganiko na upendo tulionao na wenza wetu ni imara kiasi cha kutulinda
na hatari za watu wengine wa nje ya uhusiano huo.
Hivyo katika uhusiano wa aina hiyo, inapotokea mmoja wa wenza hao akawa
anawaona watu wa nje wanaowasiliana na mwenza wake ni hatari katika
uhusiano huo, hiyo ni ishara kuwa wivu amechukua nafasi yake.
Mwandishi mashuhuri na maarufu duniani Shakespeare aliwahi kuuita wivu
kuwa ni jitu lenye kutisha lenye macho ya kijani ambalo likipata nafasi
ya kuingia kwenye uhusiano huzama na meno yake na kuuchana chana.
Ukweli kuhusu wivu ni kwamba kama kuna mwenza mmoja anakumbwa na ugonjwa
huo, ni ishara kuwa hana imani na mwenza wake yaani uaminifu wake ni wa
mashaka.
Lakini siku zote ukosefu wa uaminifu na chanzo cha wivu huwa na sababu
kama vile mwenza mmoja kutojiamini mwenyewe na kumuendea kinyume mwenza
wako hivyo na wewe kuwa na wasiwasi labda na yeye kakufanyia
ulivyomfanyia.
Lakini sababu kubwa zaidi ni watu wengi kwenye uhusiano kutokutengeneza
mipaka salama ya uhusiano wao, jambo ambalo linasaidia kujenga ukuta
katika penzi pamoja na madirisha ambayo ndiyo yatakayowaruhusu wengine
kushirikishwa.
Na hapo mkumbuke si kujenga ukuta wenye milango ambayo itawaruhusu
wapenzi wa nje wenye ushindani kuingia na kuvuruga uhusiano huo. Hali
hiyo inasababishwa na pande zote mbili kutokujua ni kitu gani
kinakubalika ndani ya uhusiano huo na kisichokubalika.
Na hapo ndipo mawazo mabaya hujengeka ambayo yanazaa wivu, mawazo kama
vile mwenza wako anakudanganya ana uhusiano na mtu mwingine nje ya
uhusiano wenu.
Jambo la muhimu hapa ni kutambua mambo yanayomfanya mtu avamiwe na ugonjwa wa wivu ili uweze kupambana nayo.
Baada ya hapo peleka mawazo yako katika kujenga uaminifu kwenye uhusiano
ulionao, ikibidi hata kupata ushauri kwa wataalamu. Lazima wote
wajifunze namna ya kuwekeana mipaka katika uhusiano, hiyo ikimaanisha
kuwa kila mmoja aheshimu mipaka ya uhusiano wa mwenzake.
0 comments:
Post a Comment