TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA
WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE
18.08.2015.
·
.MPANDA BAISKELI AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA
YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI MBARALI.
·
.JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WATU SITA WAKIWA NA POMBE HARAMU [GONGO] NA BHANGI.
KATIKA
TUKIO LA KWANZA:
MPANDA
BAISKELI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SIKU
THOBIAS (25) MKAZI WA LUNWA
WILAYANI MBARALI ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI
ISIYOFAHAMIKA ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA.
AJALI
HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 17.08.2015
MAJIRA YA SAA 21:45 USIKU HUKO
KATIKA KIJIJI CHA LUNWA-IGURUSI, KATA YA IGURUSI, TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA
MBARALI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE.
CHANZO
CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO.
UPELELEZI UNAENDELEA.
TAARIFA
ZA MISAKO:
KATIKA
MSAKO WA KWANZA, WATU WATANO WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA
1. FURAHA MALECELA (36) MKAZI WA
IPINGO 2. KENEDY MWAKANYUMA (23)
MKAZI WA KISELI 3. LISTA ANDONGOLILE
(43) MKAZI WA KISELI 4. ANYUKULILE
MWAISOBA (71) MKAZI WA IKONGO NA 5.
OSHANA ANDONGOLILE (43) MKAZI WA KISELI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA ISHIRINI [20].
WATUHUMIWA
WALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE
18.08.2015 MAJIRA YA SAA 01:37 USIKU
WA KUAMKIA LEO HUKO KATIKA VITONGOJI VYA IPINGO, KISELI NA IKONGO, KIJIJI CHA
LUALAJE, KATA YA LUALAJE, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
WATUHUMIWA NI WATUMIAJI NA WAUZAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUWAFIKISHA
MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KATIKA
MSAKO WA PILI, MTU MMOJA MKAZI WA MLOWO WILAYA YA MBOZI
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SAME KASEBELE
(18) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI UZITO WA GRAM 50.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 17.08.2015
MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI HUKO
KATIKA MTAA WA MLOWO, KATA YA MLOWO, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA
MBEYA. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI MTUHUMIWA ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA DEREVA ALIYESABABISHA AJALI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE. AIDHA ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA MATUMIZI YA POMBE HARAMU YA MOSHI NA BHANGI KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na:
[AHMED
Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment