Dustan Shekidele, Moro
My God! Mwanaume aliyetajwa kwa jina
moja la Nigar, mkazi wa Kijiji cha Kinole, Morogoro Vijijini anadaiwa
kumcharanga mapanga mkewe, Halima Abdallah (28) na kummyofoa titi kisha
kulitafuna na kumgeukia mwanaye Tausi (3) na kumtenganisha kichwa na
kiwiliwili.
Tukio hilo lililomfanya mwanahabari wetu
kufunga safari hadi kijijini hapo lilijiri Agosti 14, mwaka huu ambapo
mwanaume huyo alikuwa kwenye shamba lao la migomba ndipo alipotekeleza
unyama huo kabla ya kukamatwa na kufikishwa polisi.
Wakizungumza
na gazeti hili kijijini hapo, mashuhuda wa tukio hilo, Msimbe Joseph na
Mchilo Agustino walisikitishwa na tukio hilo na kwamba hawakujua nini
kilimpata baba Tausi hadi kufikia uamuzi huo.Baada ya kutoka kijijini
hapo, gazeti hili lilifanikiwa kuzungumza na Halima akiwa wodi namba 3
katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa sharti la kutomwambia
kama mwanaye Tausi alikuwa amechinjwa na baba yake kwani hakujua
kilichoendelea kijijini hapo baada ya kucharangwa na kuwa hoi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul.
Alisimulia kwa masikitiko: “Nimeishi na
mume wangu kwa zaidi ya miaka 10, tumebahatika kupata watoto wawili.
Siku ya tukio, nakumbuka ilikuwa saa 8:00 usiku, mume wangu alikurupuka
kitandani na kudai kuwa aliota ndoto ya ajabu.
“Aliondoka nyumbani usiku huo na kwenda kulala msikitini. Aliporejea asubuhi alichukua panga akasema twende kwenye shamba letu la migomba.
“Aliondoka nyumbani usiku huo na kwenda kulala msikitini. Aliporejea asubuhi alichukua panga akasema twende kwenye shamba letu la migomba.
“Tulipofika huko ndipo alipoanza kunishambulia kwa kunikata sehemu mbalimbali mwilini.
“Kama hiyo haitoshi, alinirukia akaning’ata titi la kushoto hadi akalinyofoa na kuanza kulitafuna kama nyama na kumeza.
“Kama hiyo haitoshi, alinirukia akaning’ata titi la kushoto hadi akalinyofoa na kuanza kulitafuna kama nyama na kumeza.
“Baada ya hapo niliokolewa na wanakijiji wakanipeleka zahanati ya kijiji ndipo nikahamishiwa hapa (Hospitali ya Morogoro).
“Bado hali yangu si nzuri kwani nasikia
maumivu makali. Nasikia baba Tausi alikamatwa anasubiri kufikishwa
mahakamani.”Kwa upande wao ndugu na wanakijiji wenzao waliendelea na
mazishi ya mtoto Tausi huku mama yake akiwa hajui kama mwanaye alipatwa
na umauti.
Gazeti hili lilipowasiliana na Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul alisema hajalipata tukio hilo
lakini alimwagiza msaidizi wake kulifuatilia na kupata ripoti kamili juu
ya tukio hilo.
SOURCE gpl
0 comments:
Post a Comment