Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
imetoa ratiba rasmi kwa vyama vya Siasa na wananchi wote itakayotumika
katika Uchaguzi Mkuu wa Serikali unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka
huu.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji wa Rufaa (Mst.) Damian
Lubuva imesema kuwa kwa Mamlaka waliyopewa kwa mujibu wa vifungu vya
35B(1), (3) (a), 37 (1) (a) na 46 (1) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,
Sura ya 343, shughuli za uchaguzi zinatarajia kuanza hivi karibuni.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa
Uteuzi wa wagombea Urais, Ubunge na Udiwani unatarajia kufanyika Agosti
21, 2015, na kampeni za Uchaguzi kwa wagombea hao zitatarajia kuanza
Agosti 22 mpaka – Oktoba 24 mwaka huu.
Halikadhalika siku ya kupiga kura
kwa wananchi wote inatarajiwa kuwa Oktoba 25, 2015 kwa wale
waliojitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.
0 comments:
Post a Comment