Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Tuesday, March 3, 2015

NEWS;MWANAUME ANAPO MCHOMA KISU HAWARA


Richard Bukos na Makongoro Oging’/Uwazi
Habari zilizolitikisa Jiji la Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita ni pamoja na ile ya mkazi wa Chamazi, Hussein Mfaume, kumchoma visu hawara yake,  Ester Thomas Ungele (30), naye kujichoma mpaka kujitoa utumbo, Uwazi limeichimba kwa kina.

Hawara akipelekwa hospitali baada ya kuchomwa kisi.
Habari zilidai kuwa, kisa hasa cha mwanaume huyo kujichukulia uamuzi huo wa kikatili ni madai ya  mwanamke huyo  kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine anayedaiwa kuwa ni dereva wa teksi.
MANENO YA SHUHUDA MKUU
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio  hilo ambaye ni mtoto wa Ester, Sarah siku hiyo, yeye na mama yake  walikuwa kwenye eneo lao la biashara ya Mama Lishe, nje ya  Ukumbi wa Vijana, Amana uliopo Ilala, Dar.

“Ghafla nilimwona Hussein akija huku usoni akionekana mtu mwenye hasira. Alimfuata mama alipokuwa na kumuuliza ni kwa nini anamfanyia dharau?”
Mume akiwa taabani baada ya kujichoma kisu.
MALUMBANO YAANZA, WAKIMBIZANA
Sarah anaendelea: “Niliona kama malumbano ya kawaida nikawa nawaangalia lakini nikashangaa kumuona Hussein akimsogelea mama na kutoa kisu.“Mama alianza kukimbia naye Hussein akamkimbiza huku bado ameshika kisu mkononi. Niliogopa sana, nikatetemeka. Nilipiga mayowe kumuombea msaada mama.

“Mama alikimbia uelekeo wa kuingia kwenye Ukumbi wa Vijana lakini kabla hajafika, Hussein alimchota mtama mama akaanguka. Ndipo Hussein alipoanza kumchoma visu mama sehemu mbalimbali za mwili na kisha kumkita nacho kichwani.”
KISU MWILINI MWAKE
Sarah tena: “Baada ya kumchoma mama visu hivyo, nilishangaa kumuona Hussein na yeye akijichoma visu sehemu mbalimbali za mwili wake lakini mwisho alijikita nacho tumboni na kuanza kukitikisa kama vile alikuwa anauchanachana utumbo wake, akaishiwa nguvu na kuanguka. Ndipo wasamaria wema wakaanza kuwasogelea.”

Sarah alisema hata yeye alisogea eneo hilo na kuwakuta wote wamepoteza fahamu huku utumbo wa mwanume ukiwa nje na damu chapachapa ikiwa imetapakaa mwilini. Wakachukuliwa na kukimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Ilala, Amana, Dar ambapo ni mita chache tu kutoka eneo la tukio.
MKE WA HUSSEIN SASA
Naye mke wa mtuhumiwa huyo aliyejitambulisha kwa jina la Zubeda Abeid alipopata nafasi ya kuzungumza na Uwazi alikuwa na ya kusema:“Ukweli taarifa hizi nimezipata kwa mshtuko mkubwa sana hali iliyonifanya nipoteze fahamu. Hussein ni mume wangu wa ndoa, alinioa mwaka 1997 kijijini kwetu, Likombora mkoani Lindi. Tuna watoto wanne.

Hawara aliyechomwa kisu.
”Mwaka 2003 tulihamia hapa Dar kutafuta maisha zaidi ya Lindi, mwenzangu kazi yake ikiwa ni kuuza kahawa pale karibu na huyo hawara yake aliyemchoma visu. Mimi ni mama wa nyumbani tu.
“Sijui walihitilafiana kitu gani na huyo hawara yake maana leo ndiyo nimejua kumbe mume wangu alikuwa na hawara. Lakini hebu soma meseji hii kwenye simu yangu, alinitumia mume wangu mwanzoni mwa mwezi huu (Februari) bila kuhofia kuwa mimi ni mke wake.”

ILIVYOSOMEKA MESEJI
 “MAMA NEEMA NAKUOMBA MESEJI HIYO ISOME PEKE YAKO NA USIMWAMBIE MTU YEYOTE. MIMI NAJIUA KWA SABABU ESTER HANITAKI. WEWE BAKI NA WATOTO,  NIMEVUMILIA KUKUFICHA NIMESHINDWA. KWA HIYO MIMI NAJINYONGA, WEWE BAKI NA WATOTO.”

Baada ya Uwazi kuzungumza na mwanamke huyo, lilibahatika kuzungumza na dalali mmoja wa magari anayefanyia shughuli zake eneo hilo lakini aliomba jina lake lisiandikwe gazetini.
“Hussein alikuwa akimtuhumu dereva taksi mmoja kwamba anaingilia penzi lake na mwanamke huyo aliyemjeruhi na amekuwa akiahidi kulipa kisasi.

Mke wa ndoa.
“Yaani leo kama jamaa angekuwepo hapa basi ndiye angekuwa wa kwanza kuchomwa visu, pengine huyu mwanamke angefuatia,” alisema dalali huyo aliyeshuhudia tukio hilo.
MGANGA MKUU
Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Dk. Shaany Mwaruka alikiri kuwapokea majeruhi hao na kusema: “Kwa sasa hali za majeruhi zinaendelea vizuri ingawa awali hali ilikuwa mbaya na kusababisha wakimbizwe chumba cha upasuaji kutokana na kisu kilichotumika kuingia sana ndani ya miili.”


0 comments: