Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Sunday, March 15, 2015

LIVE KUTOKA TAIFA:YANGA VS FC PLATNUM...mpira umeisha_YANGA 5 PLATNUM 1




Mechi imeanza kwa kasi kubwa, ila Yanga wanaonekana ndiyo wako fiti zaidi kwa kujipanga vema.

FC Platijum wanajilinda zaidi na kufanya mashambulizi ya kushitukiza na hasa kutokea pembeni.

Lakini hiyo haionyeshi kuwashitua Yanga ambao wanaendelea kucheza kwa kuonana vizuri huku wakipoteza nafasi kadhaa za kufunga kupitia kwa Haruna Niyonzima na Mrisho Ngassa.

Dakika ta 17, kipa wa FC Platinum anafanya kazi ya ziada kuokoa shuti kali la Niyonzima


Salum Telela anaifungia Yanga bao katika dakika ya 26.

Mambo yanazidi kuwa matamu kwa Yanga zaidi ya Mcharo, Niyonzima anaifungia Yanga bao la pili katika dakika ya 40 baada ya kumchambua kipa na 'kuutupia' wavuni. Ilikuwa ni baada ya Tambwe kupiga shuti kali, kipa akatema, akataka kuwagi, akalambwa chenga na Mnyarwanda huyo akafunga.

FC Platnum si wabaya, wanaonyesha nao kuchangamka na dakika ya 45, Walter Musona anafanikiwa kuwafungia bao zuri la mkwaju wa adhabu unaomshinda Barthez.

WANAKWENDA MAPUMZIKO 2-1




KIPINDI CHA PILI:



Kipindi cha pili kinaanza kwa kasi kubwa, Yanga wanaonekana kuja kwa haraka na FC Platinum wanazidiwa nguvu na kupoteza umakini.

Dk 46, Tambwe anaifungia Yanga bao la tatu, ikiwa ni dakika moja tu baada ya kuanza kwa kipindi cha pili.
 Dk 52, Yanga wanaonyesha hasira kwa kuongeza bao la nne kupitia kwa Mrisho Ngassa ambaye anamchambua kipa ikiwa ni baada ya zaidi ya basi nane kugongwa na yeye kuupachika wavuni.

Dk 56, nusura Yanga wapate bao lakini Ngassa anajaribu kuuinua juu, kipa anamshitukia na kuukoa. 
MABADILIKO: Dk 62, FC Platinum wanamtoa Wisdom Mutasa na kumuingiza super sub, Aaron Katege (Yanga inabidi wawe makini naye).

 Dk 65 Musona aliyefunga bao la Platinum, anawakosa Yanga na mpira unagonga mwamba na kuokolewa na Juma Abdul.

 MABADILIKO: Dk 69, Yanga wanamtoa Msuva na nafasi yake inachukuliwa na Mliberia Kpah Sherman.


Dk 90, Ngassa anaifungia Yanga bao la tano, mara nyingine baada ya kuiwahi krosi ya Sherman.

0 comments: