Stori: MWANDISHI WETU/Risasi
MTANGAZAJI maarufu Bongo na aliyekuwa mpenzi wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Penniel Mungilwa ‘Penny’ amedaiwa kunywa sumu kufuatia kunyang’anywa bwana na shosti yake aliyefahamika kwa jina la Diana.
Kwa mujibu wa chanzo, Penny na Diana walikuwa marafiki lakini wakatofautiana baada ya Diana kumteka akili mwanaume wa rafiki yake huyo na kumkoleza mapenzi hadi kufikia hatua ya kumtangazia ndoa.
“Diana kampagawisha mwanaume wa watu, jamaa akatangaza ndoa na hivi ninavyokwambia siku siyo nyingi Diana anaolewa hicho ndicho kikasababisha Penny apandwe na presha hadi kufikia hatua ya kunywa sumu, alikimbizwa hospitali, akalazwa lakini sasa ametoka anaendelea vizuri,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wetu alimtafuta Penny ili kujua anazungumziaje habari hizo za kunywa sumu hadi kulazwa hospitali ambapo alikanusha madai hayo.
“Sijanywa sumu, suala la mimi kulazwa huwa linatokea sababu nasumbuliwa na pumu mara kwa mara,” alisema Penny.

0 comments:
Post a Comment