Picha aliyoweka Faiza Ally Instagram ya Mhe. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ akiwa katika pozi na mwanaye Sasha.
MSANII wa filamu Faiza Ally ambaye amezaa na Mbunge wa Mbeya mjini,
Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, leo amewatolea uvuvi watu waliokuwa wakijiuliza
maswali kuhusu mwanaye Sasha na na baba yake.Kupita akaunti yake ya Instagram, Faiza ameweka picha na Mhe. Sugu akiwa na mwanaye Sasha na kuandika kuwa "Mara nyingi huwa nawapiga picha mimi mwenyewe sema tu sipendi sana kurusha kwangu"
Na kwa wale waliokuwa wanauliza maswali juu yao, Faiza amewajibu hivi: "Ni kweli kuna wakati tulikuwa hatuelewani kabisa na wala hatukuwa tunaonana lakini kwa sasa tofauti zetu zimeisha hatuna ugomvi japo hatuko pamoja"
Faiza akiwa na Mhe. Sugu enzi hizo.
"Lakini mwisho wa siku huyo ndiyo baba Sasha na mzazi siku zote
atakuwa mzazi tu, haijalishi tuna tofauti kiasi gani" Alimalizia
kuandika msanii huyo asiyeishiwa vituko.Baada ya kuwek picha hiyo wengi wa mashabiki wa Faiza walimpongeza kwa hatua hiyo huku wengine wakiwataka warudiane ili walee mtoto pamoja.
0 comments:
Post a Comment