Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Friday, March 20, 2015

KUMBE DIAMOND NA DJ WAKE ROMY JONES WAMEANZIA MBALI__CHEKI PICHA ZAO ZA UTOTO

Na Musa Mateja
Kwa sasa tunapozungumzia mastaa wa muziki wanaofanya vizuri hapa Bongo, jina la Nasibu Abdul ‘Diamond’ lazima litachukua nafasi ya kwanza kisha wengine watafuata. Ni kijana anayejituma sana na jitihada zake hizo zimemfanya awe maarufu barani Afrika.
Picha tofauti wakati wa utoto wao.
Nyuma ya mafanikio ya Diamond wapo watu wengi. Mwenyewe amekuwa akimshukuru sana mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’ kwa malezi aliyompa hadi kufikia hapo alipo leo. Ukimuacha mama yake, wapo watu wengine wengi lakini leo nataka kukupa angalau kwa uchache uhusiano uliopo kati ya Diamond na DJ wake, Romy Jones.
Katika safari ya kimuziki, Diamond na Romy wametoka mbali sana. Kwa wasiojua, wawili hawa ni ndugu kabisa, ni mtu na kaka yake kwa upande wa mama zao. Yaani  mama wa Diamond na mama wa Romy ni mtu na dada yake.
Mwandishi wa makala haya, alipata nafasi ya kuzungumza na Diamond juu maisha yake na Romy enzi za utoto wao, soma hapa chini…
Maisha ya utotoni
Diamond: “Awali Romy alikuwa akiishi Kinondoni kwa baba yake lakini kila wikiendi alikuwa anakuja Tandale, tunakula ‘good time’ kisha anaondoka. Ikafika kipindi baba yake akafariki na hapo ndipo mama wa Romy alipolazimika kurudi kwao, Tandale akamkuta dada yake (mama Diamond) akiwa na mimi. Hapo ndipo tukakua na kucheza pamoja.
“Hakuna sehemu ambayo ungemkuta Romy bila mimi kuwepo. Yalikuwa ni maisha f’lani ambayo natamani yajirudie. “Ukweli Romy alikuwa ni mkubwa kwangu lakini tuliishi kama mapacha licha ya kwamba Romy alikuwa mtundu kuliko mimi.
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Ishu ya shule ikawaje?
Kwa namna tulivyokuwa ilikuwa ngumu kupelekwa shule tofauti, tulisoma shule moja kuanzia shule ya msingi hadi sekondari.
Ubishoo ilikuwa
tangu utotoni
“Unajua sisi wazazi wetu walikuwa wa kisasa, walikuwa wanajua kutuvalisha vizuri na ndiyo maana picha nyingi za utotoni cheni, raba, jinzi na tisheti za kijanja kama kawa. Kwa hiyo huu usafi hatukuuanzia juzi wala jana, sisi tangu ‘long time’ kitambo.”
Walichopendelea zaidi
“Enzi hizo tukiwa wadogo hatukujua kama tutakuja kufanya muziki, tulifanya mambo mengi ya kitoto tu. Tulikuwa tunacheza sana mpira kama ilivyo kwa watoto wengine.”
Muziki ilikuwaje?
“Wakati tuko wadogo, nakumbuka kuanzia tukiwa shule ya msingi, mama yangu alikuwa akitupeleka sana kwenye maeneo ya burudani. Ikitokea kuna mashindano ya kuimba ‘talent show’ alikuwa akitushika mkono na kutupeleka, huko ndiko tulikoanzia mambo ya muziki.”
Mwanzo wa ustaa
Romy Jones.
Romy alipokuwa akifanyiwa ‘intaviu’ katika Kipindi cha Sporah hivi karibuni alisema: “ Wakati nilipoanza kufanya kazi ya utangazaji pale Clouds, Diamond hakuwa lolote, alikuwa akiniona kwenye TV, yeye bado anapambana na maisha ya uswahilini huku akifanya muziki.
“Wakati mimi naanza kupata zile elfu 10 na zaidi, yeye alikuwa hana hata mia. Nikawa namtoa kimtindo.
“Ikafika kipindi ndiyo nikamtambulisha Diamond kwa watangazaji wenzangu akiwemo Adam Mchomvu, nikawaambia nina mdogo wangu anaitwa Diamond anaimba, tunamsaidiaje.
“Tukarekodi nyimbo kibao zikaishia hewani. Kuna moja ya kurap tukafanya na Gez Mabovu na Gwea (wote marehemu) kisha nikaipeleka Clouds. Mchomvu alipoisikia akaipenda ikaanza kupigwa, Diamond akawa anafurahi sana. Safari ya kimuziki ikaanzia hapo na mpaka sasa mimi ni Official DJ na Tour Manager wa Diamond.



0 comments: