Musa mateja
KABAANG! Mkali wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, amedaiwa kumfumania ‘laivu’ mchumba wake Siwema akiwa kitandani na ‘serengeti boy’ wake ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, Ijumaa lina full stori.
Mkali wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.
NI MWANZAKwa mujibu wa chanzo kilichoshuhudia mwanzo mwisho, tukio hilo lilichukua nafasi Machi 15, mwaka huu maeneo ya Kitangiri jijini Mwanza ambako mrembo huyo alikuwa akiishi, baada ya Nay kupenyezewa ‘ubuyu’ kuwa mrembo huyo usiku wa Machi 14 alionekana akiponda raha ndani ya klabu moja iliyopo katika jengo la Hoteli ya Golden Crest.
“Wambeya walimpenyezea habari Nay, kesho yake asubuhi sana akatimba Mwanza kwa ndenge na kumkuta laivu Siwema akiwa na seregeti boy wake kitandani,” kilisema chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.
AMPOKONYA SIMU, AWAPIGA PICHA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, Nay baada ya kuwakuta wawili hao wakiwa katika hali ya taharuki katika chumba cha nyumba hiyo ambayo alimpangishia Siwema, alimpokonya simu mpenzi wake huyo na kuwapiga picha za ushahidi wawili hao kisha akamchukua mwanaye kurudi Dar.
SIWEMA ATOKA NA KANGA MOJA
“Siwema baada ya kuona Nay amempokonya simu, alikurupuka akiwa na kanga moja kisha kumfuata ili arejeshewe simu yake, Nay aligoma na kukwea teksi akamuacha Siwema akilalama,” kilidai chanzo hicho.
NAY MSTARABU?
“Kiukweli Nay ni mstarabu sana maana hakuonyesha hasira za aina yoyote pamoja na kwamba aliwafuma laivu, alitoka taratibu, hakufanya ugomvi wowote kama watu wengine wanavyofanya pindi wanapofumania,” kilizidi kudai chanzo chetu.
NAY AKWEA PIPA, ARUDI DAR
Chanzo hicho kilizidi kudai kuwa, baada ya Nay kufanikiwa kumuacha Siwema na jamaa yake, alikwenda Uwanja wa Ndege wa Mwanza na kupanda ndege kurejea maskani kwake jijini Dar.
“Jamaa (Nay) hakutaka kuuweka usiku, alichokifanya ni kukwea pipa na kichanga chake hadi jijini Dar na kwenda kumkabidhi mama yake,” kilisema chanzo hicho.
NAY ANASEMAJE?
Mwanahabari wetu baada ya kuzinyaka habari hizo, alimvutia ‘waya’ Nay ambapo alipopatikana na kusomewa mashtaka ya kwenda kumfumania mchumba wake, alisema hayupo tayari kuzungumzia suala hilo kwa undani lakini akadai amemchukua mwanaye mikononi mwa Siwema kutokana na mchumba wake huyo kuzidiwa na mambo yake.
“Sitaki kuzungumzia chochote kwa sababu sitaki kuonekana mbaya, ila kiukweli nilienda Mwanza na kumchukua mwanangu na hapa ninapozungumza na wewe, mwanangu yupo chini ya uangalizi wa mama yangu mzazi,” alisema Nay.
SIWEMA KAFUATA SIMU YAKE
Wakati gazeti hili linakwenda mitamboni, chanzo kilicho karibu na wawili hao kilipenyeza ubuyu kuwa Siwema ameibuka jijini Dar kwa lengo la kufuata simu yake ikidaiwa kwamba eti ina siri zake nyingi.
SIWEMA HAPATIKANI
Jitihada za kumpata Siwema kupitia simu yake ili aweze kufunguka kwa upande wake hazikuzaa matunda kwani simu yake ilikuwa mikononi mwa Nay, jitihada zinaendelea ili na yeye afunguke ukweli wa tukio hilo.
TUJIKUMBUSHE
Nay na Siwema wamedumu kwenye uhusiano kwa takriban miaka mitatu ambapo wamefanikiwa kupata mtoto huyo mmoja. Awali, Nay aliwahi kuingia kwenye mgogoro na kigogo mmoja ambaye alikuwa akimtaka mrembo huyo lakini alifanikiwa kumuweka mikononi mwake kabla ya kumfumania na serengeti boy.
0 comments:
Post a Comment