Ni wiki nyingine tulivu kabisa tunakutana tena kupitia safu hii
nikiamini umzima bukheri wa afya na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila
siku kama kawaida.
Mimi namshukuru Muumba wa mbingu na ardhi kwa kuniwezesha kutimiza majukumu yangu ya kila siku likiwemo hili la kuelimishana na kukumbushana juu ya mambo yanayogusa maisha yetu ya kimapenzi.
Mimi namshukuru Muumba wa mbingu na ardhi kwa kuniwezesha kutimiza majukumu yangu ya kila siku likiwemo hili la kuelimishana na kukumbushana juu ya mambo yanayogusa maisha yetu ya kimapenzi.
Mpenzi msomaji wangu, wiki iliyopitanilikuwa na kazi kubwa ya
kumshaurirafiki yangu ambaye aliniletea mashitaka ya mpenzi wake kutembea na
rafiki yake.
Nilipata wakati mgumu sana kwani nilipoongea na msichana akaniambia wazi
kwamba, amekuwa hapati penzialilotarajia kutoka kwa rafiki yangu.
Msichana huyo akaenda mbele zaidi na kusema kwamba, yule shemeji yake
alionesha kumjali sana kiasi kwamba siku alipomtamkia kwamba anampenda ilimuwia
ngumu kukataa.
Kuna kitu cha kujifunza hapa kwamba endapo utaishi na mpenzi wako bila
kumdhihirishia kwamba unampenda kwa dhati, akitokea mtu wa pembeni akaonyesha
kuwa kafa kaoza, tarajia kusalitiwa kama siyo kuachwa kwenye mataa.
Unapokuwa umeanzisha uhusiano namtu, utambue ana watu wengi wanaomtaka
lakini huenda anawakatalia kwa kuwa yuko na wewe, sasa ukionesha kutomjali,
hawezi kuendelea kuwa muaminifu kwako.
Atachepuka na hata kama
ataendelea kuwa na wewe ni kwa kuwa labda hana ujasiri wa kukuacha.
Ndiyo maana leo nikaona nikupe sababu ambazo zinaweza kumfanya mpenzi
wako akatembea na rafiki yako tena wakati mwingine kwa siri bila wewe kujua.
Wewe mwenyeweEndapo utakuwa umeanzisha uhusiano na mtu, wewe mwenyewe
unaweza kutengeneza mazingira ya kusalitiwa.
Usipoonesha kumpenda, kumjali, kuthamini penzi lake kisha rafiki yako
akayaonesha hayo kwake,ni rahisi sana kukupiku.
Kwa mfano, endapo umekuwa na mpenzi wako lakini hata siku moja hujawahi
kumpa zawadi au kumtoa ‘out’, siku shemeji yake (rafiki yako) akiamua kufanya
hivyo, mpenzi wako atahisi yeye ni mtu sahihi kwake.
Kujirahisi kwakeWapo ambao wanatembea na mashemeji zao kwa sababu tu ya
kujirahisi kwao.
Kwa mfano unapopendelea kuzungumza mamboya chumbani na rafiki wa mpenzi
wako unatarajia nini? Unapomvalia kihasara rafiki wa mpenzi wako lengo linakuwa
ni lipi?Mbaya zaidi ni pale utakapokuwa na mashemeji ambao hawabipiwi.
Hapanamaanisha wale ambao wakiona dalili ya kupendwa tu, wanaomba chansi
Hayo machache akili kichwani
0 comments:
Post a Comment