Kifo cha mnenguaji Mwainaisha Mohamed Mbegu “Aisha Madinda” aliyefariki jana, kimeleta utata kwa namna kilivyotokea.
KALI ZA DJ YEYO inakuletea kwa muhtasari wa namna kifo cha Aisha Madinda kilivyotokea,
hii ikiwa ni kwa mujibu wa ndugu na marafiki wa marehemu waliokusanyika
hospitali ya Mwananyamala .
Mtoto
wa kwanza wa marehemu, Feisal amesema mama yake ambaye
alikuwa haumwi chochote, aliondoka nyumbani juzi na hakurejea tena.
Feisal
anasema juzi aliongea na mama yake kwa njia ya simu kwa zaidi ya mara
tatu na akamwambia yuko Mabibo kwa rafiki yake aitwaye Samira.
Lakini
Samira anasema Aisha Madinda hakuwa kwake hiyo jana lakini alimkuta
barazani kwake (Mabibo) asubuhi ya leo akiwa hajitambui.
Samira
anasema alijitahidi kumtingisha lakini Aisha Madinda alikuwa kimya na
hivyo akaamua kuchukua bajaji na kumkimbiza hospitali ya Mwananyala.
Rafiki
huyo wa Aisha Madinda anasema alifika Mwananyamala Hospitali majira ya
saa 2 asubuhi na daktari aliyempokea akamwambia tayari mgonjwa wake
alishafariki dunia.
Samira
anasema, yeye kama alivyo Aisha Madinda, ni muathirika wa madawa ya
kulevya ambapo anaitaja hospital ya Mwananyamala ndio kliniki yao ya
kupata tiba saidizi (MAT) ya madawa ya kulevya na ndio sababu
hakumpelekea hospitali nyingine yoyote zaidi ya Mwananyamala.
Kinachoshukiwa:
Marafiki
wa Aisha Madinda ambao nao ni waathirika wa madawa ya kulevya, wanadai
Aisha Madinda alirudia utumiaji wa madawa ya kulevya na hivyo wana
mashaka kuwa alitumia kiasi kikubwa kuliko inavyohitajika na pengine
ndio sababu ya kifo chake.
Ndugu wanasemaje?
Ndugu
wa marehemu akiwepo dada yake ambaye ndio wa kwanza kuzaliwa, Amida
Mohamed Mbegu, amesema kuwa hadi sasa wameadhimia kukubali
kazi ya Mungu na hawatarajii kuufanyia upasuaji mwili wa marehemu ili
kujua chanzo cha kifo chake.
Maisha yake katika siku za hivi karibuni:
Ndugu
wa marehemu wanasema katika siku za hivi karibu, Aisha alikuwa
akiondoka nyumbani kwao Kigamboni asubuhi na kusema anaelekea kwenye
mazoezi ya Twanga Pepeta kwaajili ya onyesho la miaka 16 ya Luizer
Mbutu.
Lakini
kiongozi wa madansa wa Twanga, Danger Boy amesema kuwa Aisha
Madinda hajawahi kuonekana kwenye mazoezi ya bendi yao.
Kiongozi
wa Twanga Pepeta, Luzier Mbutu naye amekiri kuwa licha ya Aisha Madinda
kumwahidi mara kadhaa kwa njia ya simu kuwa atashiriki mazoezi, lakini
hakuwahi kutokea hata mara moja.
Mazishi yake:
Mwili wa marehemu umehifadhiwa chumba cha maiti cha Hospitali ya Mwananyamala na mazishi yatafanyika Kigamboni leo saa 10.
0 comments:
Post a Comment