Raphael Tenthani |
Pichani ni Raphael Tenthani, mwakilishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) nchini Malawi.
Aina yake ya mavazi na uvaaji wake umezua gumzo katika mitandao jamii.
Ralph amezoeleka kuonekana katika mavazi ya 'hovyo hovyo', yaliyolowa,
machakavu na yaliyotoboka huku viatu vikiwa vimeachama, nywele 'vululu
vululu' na sura ya 'kilevi'.
Mwandishi huyu wa habari hujihudhurisha alivyo katika kazi zake
mbalimbali za kuhojiana na kurusha habari bila kujali ustaarabu wa eneo
husika hata ikiwa ni kwenye zulia jekundu.
Wengi wanasema mkosoaji huyu mkubwa wa Serikali zote zilizoongozwa na
Marais ndugu, Bingu (marehemu) na Peter Mutharika, huenda anafanya hivyo
ili kutimiza masharti ya 'mganga' aliyemsaidia kupata ujasiri, akili nyingi
na kazi katika shirika kubwa la utangazaji la BBC. Wanadai ikiwa
atakiuka masharti hayo, huenda akapoteza kazi yake na kuwa 'juha'.
0 comments:
Post a Comment