
Kamanda wa kikosi cha zima moto na
uokoaji mkoani Iringa bw. bwana Kennedy Komba amewataka wananchi kuwa makini na
moto unapotokea ili kuepuka madhara mengine ambayo yanaweza kujitokeza.
Wito huo ulitolewa kwa wananchi hapo
jana katika kata ya makorongoni jirani na makorongoni geragi baada ya kikosi
cha zima moto kuuzima moto uliokuwa ukiunguza mataili ambayo yalitupwa koromgoni
na wananchi pia aliwataka wananchi kuchukua tahadhari kubwa majanga ya moto
yanapotokea.
Komba alisema,walitumia muda mrefu
kuuzima moto huo kwasababu ulikuwa mkubwa na iliwalazimu kutumia maji nyenye
dawa (form compaund) kwaajili ya kuuzima moto huo.
Alisema,watu wanatabia ya kutupa vitu
mbalimbali kwenye dampu kama chupa zenye gesi hivyo huwa ni rahisi sana
kujitokeza kwa milipuko wakati moto unapowaka ndio maana huwa tunawaambia watu
kukaa mbali na janga la moto linapotokea.
Aidha komba aliwataka wananchi kutoa
taarifa kwa kikosi cha zima moto kunapokuwepo na janga la moto ili kuokoa mali
za wananchi pia aliongeza kuwa ushirikiano wanaoupata kutoka kwea waandishi wa
habari na wananchi umewafanya wao kufanya kazi kwa haraka.
0 comments:
Post a Comment