Jumatatu hii Amber Rose na Wiz Khalifa wamesherehekea talaka yao wakiwa pamoja kwenye strip club huko Los Angeles.
Kwa mujibu wa TMZ, Wiz Khalifa amemlipa ex wake huyo [Amber Rose] kiasi cha dola 644,000 kwa ajili ya talaka hiyo na atatakiwa kutoa kiasi kingine cha dola 14,800 kwa ajili ya malezi ya mtoto wao Sebastian.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Amber Rose ameandika: “Too much fun with my Ex hubby last night & no we didn’t celebrate our divorce we celebrated our love 4 each other cuz that never goes away ,7.”
Mahusiano ya wawili hao yameonekana kuwa tofauti japo wameachana lakini wamekuwa wakishirikiana mara nyingi tofauti na mastaa wengine wanapoachana.
0 comments:
Post a Comment