MOHAMED BIN HAMMAM amesema kuwa hataki kuona jina la FIFA likiendelea kupakwa matope hivyo ameamua kujitoa kwenye kinyang’anyiro cha uraisi wa shirikisho hilo la kandanda duniani.
Bin Hammam |
BIN HAMMAM ameysasema hayo ikiwa ni muda mchache kabla ya Rais huyo wa shirikisho la mpira Barani Asia mwenye umri wa miaka 62 hajafikishwa mbele ya kamati ya maadili kujibu tuhuma za rushwa zinazomkabili.
Sepp Blatter |
Bin Hammam alikuwa apimane ubavu na Rais wa sasa wa FIFA Sepp Blatter,ambaye naye anahushishwa kwenye kashfa ya rushwa,ijapokuwa wote wamepinga kuhusika.
Madai ya Bin Hammam kujitoa kunamaanisha kuwa Blatter ndiye pekee aliyebakia katika kinyanganyiro hicho cha urais wa FIFA kitakachofanyika siku ya jumatano ijayo.
Blatter na Bin Hammam |
0 comments:
Post a Comment