BARCELONA wanatakiwa kuwa makini zaidi leo wakati watakapoikabili Manchester United inayosaka kulipiza kisasi kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa itakayochezwa kwenye Uwanja wa Wembley
VS
United, inatinga kwenye fainali hizo ikiwa na lengo la kusaka ubingwa kwa mara ya nne, pia wakiwa na hofu ya kipigo pamoja na mchezo wa pasi nyingi za Barca iliyowakuta kwenye fainali ya jijini Rome mwaka 2009 na kukubali kipigo cha mabao 2-0.
Tangu 2009 miaka miwili baadaye wanakutana tena kwenye uwanja wa Wembley, kiwanja kinachoonekana kufurahisha zaidi mabingwa hao wa Hispania wakiwa na nyota wao Lionel Messi, wakitegemea kutawala sehemu kubwa ya mchezo huo.
Lakini wakati Barcelona wakijivunia umakini wao wa kutandaza soka, watakuwa na wakati mgumu mbele ya bosi wa United, Alex Ferguson ambaye hatakubali makosa aliyoyafanya yajirudie tena.
VS
Akiwa na nyota wa England, Wayne Rooney na swahiba wake kutoka Mexico, Javier Hernandez wamekuwa ni mwiba mkali kwa mabeki wengi msimu huu.
“Hatuwaogopi Barcelona,” kiungo wa Korea Kusini, Park Ji-sung, alikuwa miongoni mwa wachezaji waliofungwa na Barcelona miaka miwili iliyopita, akiwaambia wanahabari wiki hii. “Ni moja ya timu bora kabisa duniani kwa sasa, lakini na sisi tuna ubora wetu.”
Ni wazi kuwa United ina ubora wake, lakini inahitaji kipaji cha ziada kushinda vita yake hiyo ambapo timu hizo mbili zote zimeshinda mataji hayo mara tatu na jambo la kuvutia zaidi ni kwamba ubingwa wao wa kwanza walipata kwenye Uwanja wa Wembley wa zamani.
Guardiola alikuwa miongoni mwa nyota wa Barca waliochukua ubingwa huo mwaka 1992, waliposhinda 1-0 dhidi ya Sampdoria katika muda wa nyongeza kwenye uwanja huo uliojulikana kama 'Twin Towers'.
Ukirudi nyuma mwaka 1968 United ilishinda taji lake la kwanza la Ulaya kwenye uwanja wa Wembley kwa kuibwaga Benfica kwa mabao 4-1 pia katika muda wa nyongeza.
UBORA WA KIUNGO
Ubora wa viungo Xavi na Andres Iniesta ndio uliiwezesha Hispania kutwaa Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini na wana hakika wataendelea kuibeba Barca leo.
Huku Messi atakuwa na kazi kubwa ya kuvuruga mabeki wa United kuanzia katikati ya uwanja atapokuwa akicheza bila ya majukumu yoyote.
Lakini mabingwa hao wa England wanajivunia safu yao bora ya ulinzi chini ya nahodha Nemanja Vidic na Rio Ferdinand, huku golini akiwepo mkongwe Edwin van der Sar (39), ambaye anategema kustaafu baada ya mechi hiyo.
Messi aliyefunga mabao 52 kwenye mashindano yote msimu huu, pia ndiye anayeongoza kwa ufungaji kwenye Ligi ya Mabingwa akiwa amefunga mabao 11 katika mechi 12, lakini nyota huyo wa Argentina atakuwa na msaada mkubwa kutoka kwa Pedro na David Villa.
VS
United yenye ndoto ya kulipiza kisasi cha 2009, itakuwa ikitegemea kupeleka mashambulizi yake kupitia kwa Rooney na Hernandez ‘Chicharito’ waliokuwa na mafanikio zaidi katika msimu huu ndani ya Old Trafford.
0 comments:
Post a Comment