Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Friday, May 27, 2011

KESHO MTOTO HATUMWI DUKAN LIGI YA MABINGWA ULAYA......

                           
WAKATI KESHO tunashuhudia mechi kali ya kukata na shoka katika fainali ya ligi ya ulaya UEFA  kati ya Man u na Barca,dimbani wembley ifuatayo ni historia ya timu hizo mbili katika kukipiga fainali za UEFA miaka ya nyuma

-KLABU za Barcelona na Manchester United zimeshacheza jumla ya fainali 10 tofauti za Ligi ya Mabingwa pamoja na moja iliyowakutanisha mwaka 2009 ambako Barcelona iliifunga United 2-0 jijini Rome.


MESS


Pia, walishawahi kukutana mwaka 1991 kwenye fainali ya Kombe la Washindi ambako Manchester United ilishinda 2-1.

Zifutazo ni baadhi ya fainali zilizocheza na timu hizo kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya:

BARCELONA


Berne, Mei 31 1961: BENFICA 3 BARCELONA 2

Real Madrid ilikuwa ikitawala soka ya Ulaya tangu wakati ambao michuano hiyo ilipokuwa imeanzishwa mwaka 1955, hadi pale walipofungwa na mahasimu wao Barcelona kwa jumla ya mabao 4-3 kwenye hatua ya mtoano mwezi Novemba1960 kumaliza utawala huo wa Real.

Hata hivyo Barcelona walishindwa kuvaa viatu vya Real kwenye michuano hiyo. Pamoja na kupata bao la kuongoza dakika ya 20 kupitia Sandor Kocsis dhidi ya Benfica kwenye fainali ya 1961, walimaliza mechi hiyo kwa kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa Benfica na iliwalazimu kusubili kwa mihongo mitatu kusogelea mafanikio ya Real.

Seville, Mei 7 1986: STEAUA BUCHAREST 0, BARCELONA 0

(Steaua ilishinda kwa penalti 2-0)

Robo karne imepita lakini bado jinamizi la kufanya vibaya linaendelea kuwaandama mashabiki wa Barcelona kwenye michuano hiyo ya Ulaya.

Wakiwa chini ya kocha kutoka England, Terry Venables, Barcelona walijitegeneza njia ya kipekee ya kutinga fainali ikiwa na pamoja na kuwatoa mabingwa watetezi Juventus huku wakipewa nafasi ya kuchukua taji hilo kwenye fainali iliyofanyika jijini Seville.

Hata hivyo, kipa wa Steaua, Helmut Duckadam ndiye alikuwa kikwazo kwa Barcelona baada ya kuokoa penalti zote.

London, Mei 20 1992: BARCELONA 1 SAMPDORIA 0

Hatimaye Barcelona waliona mwezi wa kutwaa ubingwa wa Kombe la Ulaya kwa mara ya mwisho kabla ya kubadilisha mfumo wa mashindano hayo na kuwa Ligi ya Mabingwa msimu uliofuta.

Nyota wa Uholanzi, Ronald Koeman alifunga bao pekee zikiwa zimebaki dakika nane za muda wa nyongeza kwenye Uwanja wa Wembley na Barcelona kutwaa taji la kwanza la michuano hiyo.

Athens, Mei 18 1994: AC MILAN 4 BARCELONA 0

Miaka miwili baada ya kutawazwa mabingwa wa Ulaya, Barcelona walikutana na dhahama ya kikosi cha AC Milan chini ya Fabio Capello kilichoshuka dimbani bila ya mabeki wake nyota Franco Baresi na Alessandro Costacurta, waliushangaza jijini la Athens, kwa kufunga mabao 3-0 baada ya dakika ya 47 huku mabao mawili yakifungwa na Daniele Massaro na moja la Dejan Savicevic.

Marcel Desailly alishindilia msumali wa mwisho na kuipa Milan taji na kumwacha kocha Johan Cruyff “dream team” wasiamini kilichotokea.

Paris, Mei 17, 2006: BARCELONA 2 ARSENAL 1

Katika dakika ya 14 kwenye Uwanja wa Stade de France, Arsenal waliocheza pungufu kwa muda wote wa mchezo baada ya kipa Jens Lehmann kuwa mchezaji wa kwanza kutolewa kwenye fainali, huku vijana hao wa London wakiwa mbele kwa bao 1-0 shukrani kwa goli la kichwa la beki  Sol Campbell.

Barcelona waliokuwa kwenye msimu mzuri walifanya mabadiliko ya kumwingiza mkongwe Henrik Larsson aliyeingia katikati ya kipindi cha pili na kutegeneza golo kwa Samuel Eto’o na Juliano Belletti kuwapa ushindi huo mnono.

Rome, Mei 27 2009: BARCELONA 2 MANCHESTER UNITED 0

Barcelona ilikuwa timu ya kwanza ya Hispania kutwaa mataji tatu moja la Ligi ya Mabingwa na mawili ya ndani wakati walipowaga mabingwa watetezi Manchester United kwenye Uwanja wa Olympic baada ya  Eto’o’ kufunga bao la kuongoza dakika ya 10.

Mechi hiyo ilikuwa ya ushindani kati ya nyota wa Barca, Lionel Messi na hasimu wake wa United, Cristiano Ronaldo, lakini mwisho wa sikuMessi aliibuka mshindi kwa kufunga bao la pili la ushindi kwa Barca akitumia kichwa zikiwa zimebaki dakika 20.

MANCHESTER UNITED

London, Mei 29 1968: MANCHESTER UNITED 4 BENFICA 1

Moja ya mechi za kuvutia zaidi kwenye michuano hiyo iliyoshudia United ikipata ushindi wa mabao 4-1 kwenye muda wa nyongeza na kuwa wafalme wapya ikiwa ni miaka 10 tangu walipopata ajari ya ndege ya Munich iliyoua wachezaji wote na kumwacha Busby Babes pekee.
CHACHIRITO

Kocha Matt Busby alitumia muhongo mzima kutengeneza kikosi kilichoweza kuibuka na ushindi kwa mabao mawili ya Bobby Charlton, aliyenusurika kwenye ajari, George Best na Brian Kidd walifunga bao moja moja.

Barcelona, Mei 26 1999: MANCHESTER UNITED 2 BAYERN MUNICH 1

United ilifanya miujiza kwenye fainali ya Ulaya kwa kupata mabao mawili kupitia kwa Teddy Sheringham na Ole Gunnar Solskjaer katika dakika mbili za nyongeza baada ya zile 90, na kuwaacha Bayern mikono mitupu pamoja na kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya sita kupitia Mario Basler.

Rais wa UEFA wakati huo, Lennart Johansson amekuwa akisumulia tukio hilo mara kwa mara kwa kuwa wakati anaamua kushuka kutoka kwenye jukwaa la VIP kwa ajili ya kuandaa kombe kwa Bayern waliokuwa wakiongoza wakati akielekea uwanjani alikuwa ubao umebadilika hivyo hakuona mabao yote mawili ya United. Pia ilikuwa siku ambayo Busby alitimiza miaka 90 ya kuzaliwa kwake.

Moscow, Mei 21 2008: MANCHESTER UNITED 1 CHELSEA 1

(Manchester United ilishinda kwa penalti 6-5)

Ushindi mwingine kwa United, usiku mwingine wa vituko kwenye jiji la Moscow na mvua kubwa iliyoshuka kwenye Uwanja wa Luzhniki ikizikutanisha timu mbili za England kucheza Russia kwa mara ya kwanza mechi hiyo ilikwenda hadi dakika 120 baada ya Ronaldo na Frank Lampard wote kufunga mabao kwenye kipindi cha kwanza.

Mechi hiyo ilihukumiwa kwa penalti. Baada ya Ronaldo kukosa penalti yake  nafasi ilikuwa kwa nahodha wa Chelsea, John Terry aliyetakiwa kufunga tu na kuipa ubingwa Chelsea, lakini aliteleza na kuupiga mpira vibaya nje. Edwin Van der Sar alimaliza kazi kwa kuokoa penalti ya Nicolas Anelka.

Rome, Mei 27, 2009 BARCELONA 2 MANCHESTER UNITED 0


--------------------


OOO

0 comments: