Watu tisa wamefariki dunia baada kundi la watu wenye silaha kuivamia ikulu ya jamhuri ya Kongo na kupambana na walinzi wa ikulu wakiwa na nia ya kumuua rais Joseph Kabila.
Kundi la watu wenye silaha wakiwa na bunduki na mapanga waliyavamia makazi ya rais wa Jamhuri ya Kongo, Jospeh Kabila wakiwa na nia ya kumuua rais huyo na kuipindua serikali yake.
Mapambano makali yaliyodumu takribani lisaa limoja yalizuka baina ya walinzi wa ikulu na kundi hilo ambapo watu saba toka kwenye kundi hilo waliuawa huku walinzi wawili wa ikulu nao wakipoteza maisha yao.
Rais Kabila na mkewe hawakuwepo ndani ya makazi hayo wakati shambulio hilo lilipotokea.
Waziri wa mawasiliano, Lambert Mende alijitokeza kwenye televisheni ya taifa na kusema kuwa hali sasa iko shwari.
"Hawa watu walitaka kumdhuru rais Kabila", alisema waziri Mende na kuongeza kuwa baadi ya watu toka kwenye kundi lililofanya shambulizi hilo waliuliwa na wengine walikamatwa na kutiwa mbaroni.
Rais Joseph Kabila alichaguliwa katika uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia mwaka 2006 na ana mpango wa kugombea tena katika uchaguzi ujao mwezi novemba mwaka huu.
Alirithi urais toka kwa baba yake, Laurent Kabila aliyeuliwa mwaka 2001.
Source- Nifahamishe
Kundi la watu wenye silaha wakiwa na bunduki na mapanga waliyavamia makazi ya rais wa Jamhuri ya Kongo, Jospeh Kabila wakiwa na nia ya kumuua rais huyo na kuipindua serikali yake.
Mapambano makali yaliyodumu takribani lisaa limoja yalizuka baina ya walinzi wa ikulu na kundi hilo ambapo watu saba toka kwenye kundi hilo waliuawa huku walinzi wawili wa ikulu nao wakipoteza maisha yao.
Rais Kabila na mkewe hawakuwepo ndani ya makazi hayo wakati shambulio hilo lilipotokea.
Rais Joseph Kabila |
"Hawa watu walitaka kumdhuru rais Kabila", alisema waziri Mende na kuongeza kuwa baadi ya watu toka kwenye kundi lililofanya shambulizi hilo waliuliwa na wengine walikamatwa na kutiwa mbaroni.
Rais Joseph Kabila alichaguliwa katika uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia mwaka 2006 na ana mpango wa kugombea tena katika uchaguzi ujao mwezi novemba mwaka huu.
Alirithi urais toka kwa baba yake, Laurent Kabila aliyeuliwa mwaka 2001.
Source- Nifahamishe
0 comments:
Post a Comment