Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Tuesday, October 12, 2010

CHADEMA WAVIMBA

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinapanga kuwasilisha malalamiko kwenye vyombo vya dola kuhusu ujumbe mfupi wa maandishi unaosambazwa katika simu za mikononi na kuwa wanaodaiwa kuleta chokochoko ya umwagaji damu.

Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, amesema, Ujumbe huo unaotoka namba +3588976578 unasomeka “Slaa ni mropokaji na mgomvi anayelumbana na vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi. Anataka damu imwagike ili mradi ashinde. Tusikubali nchi yetu iwe kama Burundi au Congo au Somalia. Hana uwezo wala sifa ya kuwa Rais. Tumwepuke Slaa kama ukoma. Tusidanganyike.”

Mnyika alisema maneno ya ujumbe huo yanashabihiana na yaliyosemwa na Mwenyekiti wa Kampeni wa CCM, Abdulrahman Kinana, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika kupongeza kauli ya Jeshi na kuwa ujumbe huo ulianza kutumwa juzi jioni na kuendelea tena saa tano usiku na jana asubuhi.

Alisema, baada ya kuchunguza, wamebaini kuwa ujumbe huo umetumwa nchini na watu wanaodaiwa ni wa propaganda wa CCM na kuitaka Tume ya Mawasiliano ya Taifa (TCRA), kubaini chanzo cha ujumbe huo.

“Ujumbe huu unaangukia katika kesi ya uchochezi, tunawapelekea polisi taarifa hii, ili waifanyie kazi kama kweli tamko lao la usalama lilikuwa la kweli. Pia Tume ambayo ndio inayodhibiti mawasiliano, wataweza kueleza umma chanzo cha ujumbe huu,” alisema Mnyika.

Lakini Kaimu Mkurugenzi wa TCRA, Dk. Raynold Mfungahema, alisema hawahusiki na usambazaji wa ujumbe kutoka simu moja kwenda kwa watu wengine, na kwamba suala hilo ni la mitandao ya simu yenyewe.

“Kwa mfano kuna wateja wa simu wanapata ujumbe mfupi wa matusi, suala kama hilo ni la mitandao husika na vyombo vya usalama. Polisi wanaweza kufuatilia chanzo cha ujumbe huo. Sisi tunafanya kazi zetu kwa misingi ya taaluma na hatuko kisiasa. Ninaweza kuwashauri Chadema wafuate utaratibu kwa kwenda Polisi,” alisema.

Alisema tatizo lililopo ni kuwa mfumo wa mawasiliano nchini bado haujawa rasmi na si kila mtu amesajili simu, hivyo kuwawia vigumu kumpata ambaye hajasajiliwa.

Kuhusu utafiti wa Redet, Mwenyekiti wa kamati ya kampeni za Chadema, Profesa Mwesiga Baregu, aliwataka viongozi wa taasisi hiyo ambayo yeye ni muasisi wake, kutenganisha masuala ya taaluma na ushabiki, kwa lengo la kulinda hadhi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Alisema wana shaka na utafiti huo, kutokana na baadhi ya wahusika kuwa na uhusiano wa karibu na mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete na tayari baadhi yao wamehamia Ikulu.

“Msimamo wa Chadema katika utafiti wa Redet, tunauona una lengo la kuandaa mazingira fulani, haiwezekani ripoti hiyo ije katikati ya kampeni,” alisema.

0 comments: