Kampuni moja huko China imeomba msamaha kwa tangazo la sabuni ambalo limezua utata kwa madai ya ubaguzi wa rangi.
Kampuni hiyo ya Qiaobi , imesema imepinga na kushtumu ubaguzi wa rangi na kuomba radhi kwa tangazo hilo ambalo limezua utata.Katika tangazo hilo,linamuonyesha mwanamume mweusi akiingiza kichwa chake kwenye mashine ya kufua na baadaye kujitoa akiwa na ngozi nyeupe ya raia wa ki-asia.
Katika taarifa hiyo waliwaomba radhi Wafriaka wote na kusema ni matumaini yao kwamba watu na vyombo vya habari hawatazingatia tangazo hilo.
0 comments:
Post a Comment