Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Monday, May 30, 2016

Habre ahukumiwa kifungo cha maisha jela

Habre alipatikana na makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu , ubakaji na utumwa wa ngono.

Aliyekuwa rais wa Chad Hissene Habre amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika kwenye uhalifu dhidi ya ubinadamu , ubakaji na utumwa wa ngono.

Hissene Habre alihusika moja kwa moja katika uhalifu huo ambao ulifanyika wakati akiwa rais wa Chad.
Waathiriwa waliokuwa ndani ya mahakama wakati wa kusomwa kwa hukumu hiyo mji Dakar nchini Senegal, walishangilia wakati jaji alimaliza kusoma hukumu.
Bwana Habre anatuhumiwa kwa kuamrisha mauaji ya watu 40,000 wakati wa utawala wake miaka ya 80, madai ambayo ameyakana
Habre alikamatwa nchini Senegal , na kupelekwa uhamishoni mwaka 2013.

0 comments: