Wakati Rais Magufuli akiendelea kujadiliwa kila kona ya dunia kutokana na maamuzi ambayo amekuwa akiyafanya ndani ya siku 30 tangu amekuwa Rais, Kenya kuna stori ambayo iko tofauti kidogo kumhusu Rais Kenyatta na safari zake nje ya nchi.
Mitandaoni kuna picha inayoonesha bango linalomkaribisha Kenya Rais Kenyatta, limeandikwa hivi >>>> ‘KARIBU KENYA‘ <<<
Lakini hiyo ‘karibu’ yenyewe inawezekana
isiwe na maana ya moja kwa moja kutokana na rekodi za safari za Rais
huyo nje ya nchi ndani ya miaka mitatu ya Urais wake… rekodi zinaonesha
Rais Kenyatta ameongoza kwa kusafiri nje ya nchi mara 43 ndani ya miaka mitatu kwenye Urais wakati Rais Mstaafu, Mwai Kibaki alisafiri mara 30 ndani ya miaka 10 ya Urais wake.
Safari ya mwisho ya Rais Kenyatta alienda South Africa na Ufaransa…
Ripoti ya Serikali imesema japo wanaokosoa safari hizo ni wengi lakini
bado kuna umuhimu Rais huyo kusafiri nje ya nchi mara kwa mara.
0 comments:
Post a Comment