Unaweza kukosea ukaomba radhi lakini
watu wasiwe wepesi kukusamehe au kukuelewa kwamba umejikwaa kibinadamu…
utata na kelele ziliibuka kwenye stage ya Planet Hollywood, Las Vegas
Marekani saa chache zilizopita.
Noma zaidi ni kwamba ishu haikuishia
kwenye stage wala ukumbini, watu wakaingia mitandaoni kila mmoja
akiongea la kwake huku wengi wakionekana kama hawajachukulia poa kosa la
MC wa shughuli hiyo, Steve Harvey.
Ishu ilikuwa ni kosa la MC huyo kumtaja mrembo Ariadna Gutierrez Arévalo kutoka Colombia
kuwa ndiye mshindi, akavalishwa Taji na shangwe zikaanza… sekunde
chache jamaa akaomba radhi kwamba hilo Taji sio lake, maana yake ni
kwamba mrembo huyo sio mshindi, ila mshindi mwenyewe ni mrembo Pia Alonzo Wurtzbach kutoka Ufilipino, na Ariadna kutoka Colombia ni mrembo kwenye nafasi ya pili Miss Universe 2015.
Kipande cha video na tukio lote hivi hapa mtu wangu kama ulipitwa na hii
0 comments:
Post a Comment