LEO Man United imeshushiwa kipigo chake cha 4 mfululuzo na Stoke
City walioshinda 2-0 katika Mechi ya Ligi Kuu England na kumfanya kila
Shabiki wa Timu hiyo kumchukia Meneja Louis van Gaal na kutaka atimuluwe
haraka.
Katika Mechi hii ambayo Kepteni wa Man United Wayne Rooney alianza
Benchi, Stoke walifunga Bao lao la kwanza Dakika ya 19 baada ya Pasi ya
Geoff Camerok kwa Johnson kunaswa na Mchezaji wa Man United Memphis
Depay lakini Kichwa chake hafifu cha kumrudishia Kipa wake De Gea
kilitua kwa Johnson ambae haraka alimpasia Bojan Krkic na kufunga Bao
laini.
Stoke City walipiga Bao lao la Pili Dakika ya 26 kupitia Marko
Arnautovic baada ya Frikiki ya Bojan Krkic kuzuiwa na Ukuta wa Man
United na kutua kwake na kuachia Shuti toka Mita 20.
Hadi Mapumziko Stoke 2 Man United Kipindi cha Pili Man United
walimtoa Depay na kumuingiza Rooney na kidogo juu na kukosa Bao kadhaa
na Mechi kwisha kwa 2-0.
Jumatatu Usiku Man United wako Kwao Old Trafford kucheza na Chelsea katika Mechi nyingine ya Ligi.
VIKOSI:
Stoke City: Butland; Johnson, Shawcross, Wollscheid, Pieters; Cameron, Whelan; Shaqiri, Krkic, Afellay; Arnautovic
Akiba: Joselu, Wilson, van Ginkel, Adam, Diouf, Walters, Haugaard.
Man United: De Gea; Jones, Smalling, Blind, Young; Carrick, Ander Herrera; Mata, Fellaini, Depay; Martial
Akiba: Rooney, Romero, Schneiderlin, Varela, McNair, Borthwick-Jackson, Andreas Pereira.
REFA: Kevin Friend
0 comments:
Post a Comment