Kila mpenda soka anasubiria kuona mwaka 2015 utamalizikaje kwa kocha wa klabu ya Manchester United Louis van Gaal kuendelea kuwa Man United, Kwani Van Gaal kwa
sasa anahusishwa kufukuzwa kazi wakati wowote. Mengi yanachochea uvumi
huo kuwa upo karibu kutimia, ukizingatia mtendaji mkuu wa Man United yupo kimya kwa muda mrefu bila kutoa kauli yoyote.
Wazungu ni miongoni mwa watu wanaopenda kutunza rekodi zao zisivunjwe, December 26 kipigo cha Man United cha goli 2-0 kutoka kwa Stoke City, kinavunja rekodi ya Man United iliyodumu kwa miaka 54, katika historia Man United haijawahi kufungwa mechi nne mfululizo, mara ya mwisho kutokea hivyo ilikuwa mwaka 1961.
Hivyo Louis van Gaal anaingia katika rekodi ya David Moyes aliyevunja rekodi ya Man United ya kufungwa mechi tatu mfululizo wakati mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa mwaka 2001. Moyes hadi anafukuzwa Man United alikuwa kavunja rekodi za Man United zaidi ya 10.
0 comments:
Post a Comment