Hii ndio list mpya ya wanasoka kumi wa Afrika matajiri 2015 ….
Headlines za mishahara yao mikubwa
wanayolipwa katika soka najua umeshaizoea kwa sasa mtu wangu, katika
pita pita zangu mtandaoni nikakutana na list mpya ya wanasoka matajiri
barani Afrika, katika list hii hakuna sura ngeni sana bado watu
wameendelea kumiliki utajiri wao kama kawaida. List hii inaoongozwa na Samuel Eto’o jamaa ambaye amewahi kutwaa tuzo ya mcheza bora wa Afrika mara ndio anaongoza list hii.
10- Kiungo wa kimataifa wa Ghana ambaye amewahi kutamba katika vilabu vya Inter Milan, AC Milan, Sunderland na sasa anachezea klabu ya Al Ittihad ya Saudi Arabia Sulley Muntari ndio anashika nafasi ya 10 akiwa na urajiri wa dola milioni 40.
9- Kolo Toure aliwahi kucheza katika klabu ya Arsenal, Man City na sasa Liverpool, yeye anatajwa kuwa na utajiri wa dola milioni 43.
8- John Obi Mikel ni kungo wa kimataifa wa Nigeria anayekipiga katika klabu ya Chelsea ya Uingereza anatajwa kuwa na utajiri unaofikia dola milioni 50.
7- Licha ya kuwa kwa sasa hana timu baada ya kocha wa klabu ya Tottenham Hotspurs kutomjumuisha katika list ya wachezaji wake wa mashindano Emmanuel Adebayor anapokea mshahara wa bure bila kucheza na anatajwa kuwa na utajiri wa dola milioni 57.
6- Baada ya kutamba katika vilabu vya Chelsea, AC Milan ya Italia na sasa Panathinaïkos ya Ugiriki Michael Essien anatajwa kuwa na utajiri wa dola milioni 70.
5- Licha ya kuwa amestaafu soka miaka kadhaa nyuma mkali wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Nigeria Kanu Nwankwo bado yupo katika headlines na utajiri wake dola milioni 100.
4- Austin Jay Jay Okocha
ni mkali mwingine wa soka aliyetundika daluga miaka kadhaa nyuma lakini
katika list za utajiri, yeye ana utajiri wa dola milioni 150.
3- Didier Drogba ambaye amecheza kwa mafanikio ndani ya klabu ya Chelsea ya Uingereza, kwa sasa anakipiga katika klabu ya Montreal. Drogba ana utajiri wa dola milioni 155.
2- Licha ya kuwa jamaa aliwahi kufeli majaribio ya kujiuna na klabu ya Arsenal ya Uingereza, hiyo haikumkatisha tamaa na sasa anacheza katika klabu ya Manchester City akliyojiunga nayo akitokea FC Barcelona. Yaya Toure ambaye ni mdogo wa Kolo Toure ana utajiri wa dola milioni 170.
1- Samuel Eto’o ambaye amewahi kucheza katika vilabu vya FC Barcelona, Inter Milan, aliwahi kuingia katika headlines za kuwa mchezaji anayeongoza kwa kulipwa mshahara mkubwa duniani. Eto’o ndio anaongoza list hii kwa kuwa na utajiri wa dola milioni 202.
0 comments:
Post a Comment